WANANCHI KATAVI WAPONGEZA HOTUBA YA RAIS
Na.Issack Gerald-Katavi
BAADHI
Ya wakazi Mkoani Katavi wamepongeza agizo la
Rais John Pombe Magufuli kwa wakuu wa Mikoa Kuhakikisha Kila mtanzania
anafanya Kazi.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi |
Wakizungumza
na P5 TANZANIA MEDIA baada ya Zoezi
la Kuapishwa kwa wakuu wa Mikoa 26
walioteuliwa,wakazi hao wamesema hotuba ya Rais Magufuli inalenga Kupunguza
Malalamiko kwa serikali yanayotokana na watu wasiofanya kazi kwa kutegemea
Misaada ya Serikali.
Katika
hotuba yake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli
amewataka wakuu hao wa Mikoa Kusimamia shughuli za Maendeleo kwa Kila mwananchi
Kufanya Kazi badala ya Kukaa vijiweni na Kucheza Michezo ya pulu Muda ya Kazi.
Aliwataka
wananchi watakokamatwa wakicheza michezo
ikiwemo pulu muda wa kazi,wakamatwe na wawekwe ndani hata kwa masaa mawili ili
kuleta nidamu ya uwajibikaji.
Comments