ZAIDI YA WALIMU 3 WAFUNDISHA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU KATIKA UBAO MMOJA,DARASA MOJA WAKATI MMOJA MANISPAA YA MPANDA
Na.Issack Gerald-Mpanda
ZAIDI ya walimu watatu wamekuwa
wakifundisha wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya msingi Azimio katika
darasa moja na ubao mmoja kwa darasa la kwanza hadi la saba kwa miaka saba
sasa.
Hayo yamebainishwa na walimu wa shule
ya Msingi Azimio akiwemo mwalimu mkuu wa Shule hiyo Mwl.Beno Mahema ambapo imebainika
kuwa miongoni mwa chanzo cha hali hiyo ni Mkandarasi kufunga madarasa akishinikiza
kulipwa zaidi ya milioni 28 anazodai.
Kaimu Mkurugenzi Manispaa ya Mpanda
Bw.Lauteri Kanoni amekiri kuwepo hali hiyo na amesema kuwa Alhamisi ya Februari
4 mwaka huu wanatarajia kufanya mazungumzo baina ya uongozi wa Manispaa na
Mkandarasi ili pesa inayodaiwa Manispaa zilipwe na madarasa yaruhusiwe kutumiwa
na wanafunzi.
Mpaka sasa kuna Jumla ya Wanafunzi wenye
ulemavu 18,walimu 4 ambapo hata hivyo katika mpango wa Rais wa elimu bure
wametengewa shilingi laki tatu kwa ajiri ya chakula.
Kwa upande wake Mkandarasai wa
Kampuni ya Mwandoya Investment Bw.Paul Luguyashi ameendelea kusemakuwa
hataruhusu madarasa yatumiwe na wanafunzi mpaka atakapopewa malipo yake ya
zaidi ya Shilingi milioni 28 kwa sasa.
Kwa mjibu wa Mkataba wa
makubaliano,mkandarasi huyu ilitakiwa alipwe shilingi milioni 32 kama sehemu ya
mkataba wote baada ya kukamilisha ujenzi wa majengo mwezi Aprili mwaka 2014
baada ya kupewa tenda hiyo mwaka 2013.
Kwa hiyo kutokana na malimbikizo ya deni
la Shilingi milioni 5 kutoka mwaka 2014,ilizidi kuongezeka pamoja na riba yake kutoka
milioni 5 hadi kufikia zaidi ya Shilingi milioni 28 anazodai hadi sasa.
Hata hivyo Bw.Lunguya ameendelea
kusisitiza kuwa katu hatofungua madarasa hayo ikiwa hatalipwa pesa yake
anayodai.
Katika hatua nyingine,wazazi wenye
watoto wenye ulemavu Mkoani Katavi wametakiwa kuwapeleka shuleni ili wakapate
haki yao ya elimu kama walivyo watoto ambao siyo walemavu.
Wanafunzi walemavu walipo katika
shule ya msingi Azimio ni wasioona,wasiosikia,wenye ulemavu wa akili na viungo
ambpo kwa Mkoa wa Katavi zipo shule karibu tano zenye watoto wenye mahitaji
maalumu ambapo kwa Manispaa ya Mpanda mbali na Azimio shuleni nyingine ni Shule
ya Msingi Nyerere yenye wanafunzi wenye mtindio wa ubongo.
Hata hivyo wanafunzi wote wawili waliofanya mtihani mwaka 2015 walifaulu kwa daraja B na C na kuwa miongoni mwa wanafunzi waliosababisha Manispaa ya Mpanda kuongoza kwa miaka miwili mfululizo kitaifa katika matokeo ya darasa la saba.
Hata hivyo wanafunzi wote wawili waliofanya mtihani mwaka 2015 walifaulu kwa daraja B na C na kuwa miongoni mwa wanafunzi waliosababisha Manispaa ya Mpanda kuongoza kwa miaka miwili mfululizo kitaifa katika matokeo ya darasa la saba.
Mshirikishe mwenzako kasha toa maoni yako mdau wangu kupitia hapahapa P5 TANZANIA
MEDIA au geraldissack@gmail.com
Comments