MRATIBU ELIMU KATA WILAYANI MPANDA AUA SABABU WIVU WA MAPENZI ASHIKILIWA NA POLISI KATAVI.


Na.Issack Gerald-Mpanda
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Gidison Visent(32), mkazi wa Katuma aliuawa kwa kuchomwa na kisu kifuani na Mohamed Muna (59) mratibu elimu Kata mkazi wa Katuma.

Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhairi Kidavashairi amesema kuwa tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 27.01.2016 majira ya saa mbili na nusu usiku katika Kitongoji cha Mashineni kijiji na Kata ya ya Katuma Tarafa ya Mwese Wilayani Mpanda Mkoani Katavi.
 Kamanda Kidavashari,amesema kuwa mtuhumiwa alimkuta marehemu akiwa ndani ya nyumba yake huku akiwa anafanya mapenzi na mke wake aliyejulikana kwa jina la Ester Kasansa Chuki(36) mkazi wa Katuma.
Bw.Muna alipogonga mlango,marehemu alitoka nje na kuanza kupambana naye ambapo mtuhumiwa ambaye ni Muna alimchoma kisu kifuani na kukimbia.
Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi.
Hata hivyo Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa mahojiano zaidi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika kujibu tuhuma inayomkabili.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA