WAENDESHA VYOMBO VYA MOTO BARABARANI MKOANI KATAVI WALIZWA FAINI MIL.15.6 KWA MWEZI MMOJA WATUNISHA MFUKO WA SERIKALI.


Na .Issack Gerald-Katavi
Jumla ya Shilingi(15,600,000) Milioni kumi na tano na laki sita zimepatikana kama tozo ya makosa 576 yaliyotokana na waendesha vyombo vya moto kukiuka sheria za usalama barabarani kwa kipindi cha mwezi Januari hadi Februari mwaka huu.
                                                

Taarifa hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Oparesheni ambaye pia ndiye kaimu kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Rashid Mohamed wakati akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba na Mpanda Radio Ofisini Kwake.
Katika taarifa hiyo,imeonekana kuwa  idadi ya wanaoendesha vyombo vya usafiri bila leseni imekuwa kubwa na kufikia 270 kuliko makosa mengine ambapo makosa yenye idadi kidogo ni ulevi.
Aidha Katika taarifa hiyo inaonesha kuwa makosa yaliyotokana na kutovaa kofia ngumu(Helmeti) ni 50 ,wasiokuwa na bima 70,wasiokuwa na Leseni ya usafirishaji 36,Ubovu wa vyombo vya moto 126,kukataa kusimama 28,kuzidisha abiria kwenye gari 14,kubeba abilia wawili kwenye pikipiki moja 03,kutofunga mkanda 09 kutofuata masharti ya usalama barabarani 112 na ulevi 01.
Kamanda wa polisi Mkoani Katavi,amewaasa wamiliki wa vyombo vya moto kuendelea kufuata masharti ya usalama barabarani.
Wiki iliyopita ya Februari 19,Mkuu wa jeshi la Polisi Nchini Inspecta General wa Polisi Ernest Mangu aliwaagiza makamanda wote wa polisi Nchini kuhakikisha wanapambana na waendesha vyombo vya usalama barabarani hususani Waendesha Pikipiki(Bodaboda) ili kukomesha ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani.
Alisema kuwa makosa yasiyotakiwa kufanywa na bodaboda ni pamoja na kubeba abiria zaidi ya mmoja katika pikipiki moja,kuendesha bila kuvaa Helimeti(Kofia Ngumu) na kupita sehemu ambazo hazitakiwi kupita kama sehemu zenye taa nyekundu.
Hata hivyo mara kadhaa waendesha vyombo vya usafiri Mkoani Katavi wakiwemo bodaboda wamekuwa wakilalamika kubandikiziwa makosa sambamba na kuombwa rushwa ambapo wamekuwa wakiogopa kuripoti matukio hayo kutokana na wahusika wakuu wanaoomba rushwa ikiwa ni maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la polisi.
Mpaka sasa mwezi Februari pekee Askari watatu wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA