MZIMU WA RUSHWA WAENDELEA KUWATESA POLISI KATAVI,ASKARI WA JESHI LA POLISI MWINGINE MBARONI KATAVI KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA
Na.Issack
Gerald-Katavi
Askari wa jeshi la polisi Mkoani
Katavi PC.G.451 Peter Exavery ameshitakiwa katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda
kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya shilingi laki moja (100,000=/) kutoka kwa mzee
aliyefahamika kwa jina la Ruchege Mambalo ili kumfutia tuhuma ya mkumjeruhi
mtoto wake Lutobhisha Mambalo.
Akito taarifa kwa vyombo vya
habari,wakili na mwendesha mashtaka wa Takukuru Mkoani Katavi Bw.Bahati Stafu
Haule,amesema kuwa tukio la askari wa jeshi la polisi Bw. Peter Exavery Kashuta
kushawishi kuomba na kupokea rushwa,lilitokea mnamo Februari 09 katika Kitongoji
cha Lwega kwenye mgahawa wa Lwega,kijiji cha Lwega Namba 7A,Kata ya Mwese Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda Vijijini.
Bw. Haule amesema kuwa,Manamo
Februari 10,2016,Tume ya kupambana na kuzuia Rushwa Takukuru Mkoani Katavi
lipokea taarifa kutoka kwa Ruchege Mambalo aliyewekwa mahabusu katika kituo
kidogo cha polisi Mwese Februari 09,2016 kwa tuhuma ya kumpiga mtoto waked Lutobhisha
Mbambalo amabaye ana matatizo ya ya akili alipotaka kumchoma kisu baba yake
ambapo katika harakati za kujiokoa,Luchege mambalo alichukua jiwe na kumpiga
mtoto huo usoni ambapo mtoto huyo alikimbilia haraka kituo cha pilisi Mwese kutoa
taarifa.
Amesema kuwa wakati Bw.Mambalo
akimtafuta mtoto wake ali mkuta mtoto huyoakiwa na askari Peter Exavery Kashuta
ambapo baada ya mzazi wa mtoto huyo kufika askari huyo alishawishi mzee huyo
kupewa laki saba (700,000/= ili amwachie huru na kumfutia tuhuma ya kujeruhi.
Aidha,Bw. Haule alifafanua kuwa baada
ya taratibu za jeshi la polisi kukamilika Februari 17,2016,mtuhumiwa
alifikishwa mahakamani katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda mbele ya Mh.Chiganga
Tengwa hakimu mfawidhi mkazi wa Wilaya na kufunguliwa kesi ya jinai
Namba.61/02/2016 na kusomewa mashtaka mawili ambayo ni Kuomba au kushawishi rushwa
ya shilingi laki saba(700,000/=) huku shtaka la pili likiwa ni kupokea rushwa
ya shilingi laki moja (100,000) jambo ambalo lilikuwa na kinyume au matakwa ya
mwajiri wake kwa mjibu wa kifungu 15(1)(a) cha sheria ya kuzuia na kupambana na
Rushwa na 11/2007.
Hata hivyo aliachiwa kwa dhamana ya
kukidhi matakwa ya dhamana alizoweka mahakamani hapo ambazo ni mdhamini mmoja
mwenye hati ya au dhamana ya fedha taslimu milioni bili(2,000.000/=) na
kutosafiri nje ya Mkoa wa Katavi bila kibali cha Mahakama ya Wilaya.
Aidha,Takukuru Mkoani Katavi imetoa
angalizo na wananchi na watumishi wote wa umma kujiepusha na vitendo vya rushwa
huku jeshi la polisi likitakiwa kutambua kulinda usalama wa raia ikiwa ni
pamoja na fedha.
Februari 16 mwaka huu,Mwanasheria
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Falhati Seif Khatibu na askari magereza wawili wa gereza
la mahabusu Mpanda walifikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa
wa mauaji ya mlemavu wa ngozi albino.
Vitendo hivi mpaka lini?toa maoni kwa facebook ni Issack
Gerald,Sauti Ya Katavi na Blog P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Asante kwa kuendelea kuchagu P5 TANZANIA MEDIA,Mshirikishe
na mwenzio.
Comments