MKUU WA WILAYA YA MLELE ATOA SIKU 4 KWA MAAFISA HALMASHAURI ZA WILAYA ZA NSIMBO,MPIMBWE NA MLELE WAWE WAMEKABIDHI TAARIFA YA MADAWATI SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI
Na. Agness Mnubi-Nsimbo
MAAFISA tarafa,Watendaji wa kata na
vijiji wa Halmashauri za Nsimbo,Mlele na Mpimbwe wamepewa siku 4 za kutembelea
shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Halmashauri zao ili kubaini
upungufu wa madawati.
Agizo hilo limetolewa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali Mstaafu Issa
Suleiman Njiku katika kikao cha kamati ya ushauri ya Wilaya ya Mlele
kilichofanyika katika Halmashauri ya Nsimbo,na kuwataka ifikapo February 12 kutoa
taarifa za upungufu wa madawati.
Amesema wanatakiwa kushirikiana ili
kuzunguka katika shule za sekondari na msingi kufahamu idadi ya madawati yaliyopo na pungufu
.
Amesema ifikapo february 28
Halamashauri hizo zinatakiwa kuwa zimetatua changamoto ya upungufu wa madawati,
huku Mkoa ukizitaka Halmashauri zote kutataua tatizo hilo ifikapo mwishoni
mwa mwezi machi mwaka huu.
Halmashauri zote nchini
zinatakiwa kutekeleza agizo la Serikali
kuwa hakuna mwanafuzi anayetakiwa kukaa chini ifikapo juni 30.
Comments