ASILIMIA 10 YA WATANZANIA WANAMILIKI UCHUMI WA NCHI
Na.Issack
Gerald-Dodoma
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili kufikia lengo la
kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Taarifa
zilizopo zinaonyesha ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa
nchi na sera hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi
wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na kufaidika
na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Waziri
Mkuu amesema maeneo yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya
haraka na yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji,
uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na usafirishaji.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kwanza wa
Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika kwenye ukumbi wa kituo
cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Alisema
Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya
uchumi wa nchi yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia
alizindua Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua mkutano huo, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista
Mhagama alisema hadi sasa mikoa 20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye
halamhashauri zake na imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye
Mweyekiti wa Baraza la Taifa la
Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia ya sasa
imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia masoko au
kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia Watanzania kwa
kuwaunganisha na masoko.
Comments