MATUKIO YA WIKI NDANI NA NJE YA KATAVI KUANZIA FEBRUARI 15—20,2016.
MATUKIO YA WIKI NDANI NA NJE YA
KATAVI KUANZIA FEBRUARI 15—20,2016.
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
February 17, 2016
Na.Issack Gerald-Katavi
Watu
watano akiwemo Mwanasheria Mkuu Mkoani Katavi Bw. Falhati Seif Khatibu (45),wamefikishwa katika mahakama ya
Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa Alex Manyanza Enock (27) Mkazi wa majimoto
aliyekuwa anakabiliwa na kesi NA. MTO/IR/76/2015 ya kujaribu kuua mlemavu wa
Ngozi Albino Limi Luchoma(30) mkazi wa kijiji cha Mawiti kata ya Majimoto
Wilayani Mlele.
Kaimu
kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Rashid Mohamed,amewataja watuhumiwa kwa ujumla
kuwa ni A. 287 Sajenti John Musa (50) mkazi wa mtaa wa mji mwema Wilayani
Mpanda, A. 5385 Sajenti Deogartius Katani (50) Mkazi wa mtaa wa Kigamboni
Wilaya ya Mpanda wa gereza la mahabusu Mpanda.
Kamanda
pia amewataja wengine wanaotuhumiwa kuwa ni Mwanasheria mkuu wa Mkoa wa Katavi Falhati Seif
Khatibu (45) mkazi wa maeneo ya Msakila Shule ya Msingi ,Masanja Kasinje
Kasala(33) mkazi wa Kakese Mkwajuni Wilayani Mpanda pamoja na Ngassa Mashindike
(37) mkazi wa Majimoto Wiayani Mlele.
Kamanda
Mohamed amesema kuwa mnamo 19.01.2016 majira ya saa 09:30 asubuhi,Jeshi la
Polisi Mkoani Katavi lilipokea taarifa toka kwa raia wema kuwa mtuhumiwa Alex Manyanza Enock hayupo gereza la mahabusu
Mpanda.
Baada
ya taarifa hizo kupokelewa,jeshi la polisi lilianza upelelezi na kubaini kuwa
mtuhumiwa huyo alitoroka tangu tarehe 12.10.2015 katika gereza la mahabusu
Mpanda ambapo awali mtuhumiwa huyo aliwahi kutoroka akitumikia kifungo cha
miaka 5 kwa kosa la wizi wa mifugo katika gereza la kilimo la Kalilankulukulu
kabla ya kukamatwa kwa kesi hii ya kujaribu kuua.
Kamanda
ameendelea kufafanua kuwa,ilipofika 21.01.2016 wakati jeshi la polisi
likiendelea na upelelezi wa kesi hiyo,zilipokelewa taarifa za kuwa mtuhumiwa
Alex Manyanza Enock anapatikana Mkoani Rukwa ambapobaada ya
ufuatiliaji,mtuhumiwa alipatikana akiwa amejificha katika kijiji cha Kipande
Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa.
Katika
mahojiano ya kina,mtuhumiwa Bw. Alex Manyanza Enock alieleza jinsi
alivyofanikishiwa mipango ya kutoroka gerezani akimtaja mjomba wake Bw.Masanja
Kasinje Kasala pamoja na rafiki yake Ngassa Mashindike ambao naobaada ya
kukamatwa walikiri kufanya mipango ya kumtorosha mtuhumiwa kwa lengo la
kuwafanya watuhumiwa wengine katika kesi yao ya kujaribu kuua kutotiwa hatianki
akiwemo mjomba wake walioko pamoja katika kesi hiyo Bw.Masunga Kashinje.
Mtuhumiwa
alieleza kuwa waliwashirikisha askari magereza wawili ambao ni A. 287 Sajenti
John Musa Masagula na A. 5385 Sajenti
Deogratius Katani wote wakazi wa kituo cha kazi gereza la mahabusu Mpanda ambao
walipatiwa kiasi cha Shilingi milioni moja(1,000,000/= ) ili kumwezesha
mtuhumiwa kutoroka.
Pia
walimtaja mwanasheria mkuu wa serikali ya Mkoa wa Katavi Bw. Falhati Seif Khatibu
ambapo walidai walimpatia kiasi cha shilingi milioni mbili
(2,000,000/=)ili kumwondolea shitaka mtumiwa Masunga Kashinje baada ya kuwa
mtuhumiwa Alex Manyanza Enock amefanikiwa kutoroka.
Hata
hivyo,Kamanda wa polisi Mkoani Katavi ametoa wito kwa watumishi wa umma na wale
wa sekta binafsi kufanya kazi kwa kufuata misingi ya utumishi huku wakiendelea
kuihudumia jamii kwa ukaribu.
Wednesday,
17 February 2016
WATUMISHI WA UMMA
WATAKIWA KUTOFANYA KAZI KWA NIDHAMU YA WOGA,MABILIONI YAOMBWA KUIDHINISHWA
KUFANIKISHA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI MPANDA
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
February 17, 2016
Na.Issack
Gerald-Mpanda
Watumishi wa umma Wilayani Mpanda
Mkoani Katavi,wametakiwa kutofanya kazi kwa nidhamu ya woga na badala yake
watumie taaaluma waliyoisomea.
Wito huo umetolewa Siku ya Jumanne Februari 17 na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima kikao cha kamati ya ushauri ambacho kimefanyika kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kikao ambacho kimefanyika jana katika ukumbi wa iadara ya maji Mjini Mpanda.
Wito huo umetolewa Siku ya Jumanne Februari 17 na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza Mwamlima kikao cha kamati ya ushauri ambacho kimefanyika kwa ajili ya kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 kikao ambacho kimefanyika jana katika ukumbi wa iadara ya maji Mjini Mpanda.
Kikao hicho ambacho kimefanyika
ukmbi wa idara ya maji kinawahusisha viongozi na wakuu wa idara mbalimbali
wakiwemo Wakurugenzi ngazi ya Wilaya na Mkoa.
Akiwasilisha
taarifa katika kikoa hicho cha kupitisha mpangao wa bajeti kwa mwaka wa fedha
2016/2017,Mchumi wa Manispaa ya Mpanda Bi.Mary Kanumba,katika taarifa yake
ameiomba serikali kuidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 23.8. kwa ajili ya
kuekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na shughuli nyingine za kiutawala na
maendeleo.
Amesema
kuwa,Shilingi Bil.19.3 ni kwa ajili kwa bajeti ya kawaida na Shilingi Bil.4.4
nje ya komo wa bajeti.
Bi.Kanumba
Mapato ya ndani katika Manispaa,amesema kuwa pato limeongezeka kutoka Shilingi
Bil.1.9 hadi Shilingi Bil.2.3 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 18.5
ambapo ongezeko hilo limechangiwa na vyanzo mbalimbali vya mapato vikiwemo kodi ya majengo,ushuru wa zao la
tumbaku,leseni za biashara,minada na ushuru wa vileo.
Kwa
upande wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda katika mpango wa bajeti ya mwaka wa
fedha 2016/2017,katika taarifa ambayo imesomwa na Mchumi wa Halmshauri ya hiyo
Bw.Filemon Mrageri,Halmshauri ya Mpanda imeomba kuidhinishiwa Shilingi Bilioni
Bil 31 Mil.584 laki moja thelathini na sita elfu mia saba na arobaini
(31,584,136,740) kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo iliyokusudiwa.
Hata
hivyo,bajeti ya malipo ya mishahara ya wafanyakazi imeonekana kuongezeka kwa
kiasi kikubwa miongoni mwa sababu ikiwa ni utanuzi wa mipaka ya utawala na
ajira mpya kwa watumishi katika Halmashauri zote za Manispaa ya Wilaya ya
Mpanda.
Kikao
hicho muhimu katika Halimashauri,kimeshirikisha Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Pazza
Mwamlima ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao,wakurugenzi watendaji wa Halmashauri
za Manispaa na Wilaya ya Mpanda,wakuu wa idara mbalimbali katika katika
halimshauri zote,watendaji wa kata na baadhi ya viongozi kutoka Idara katika
ngazi ya Mkoa akiwemo Meneja wa Idara ya Maji Mpanda Injinia Zacharia Nyanda na
Meneja Mpya wa wa Kwanza wa Shirika la Umeme Tanzania Tanesco Mkoa wa
Katavi.
TAMKO LA IDARA YA MAJI KATAVI
KUPITIA KIKAO CHA TAREHE 16 FEBRUARI CHA KUPITISHA MPANGO WA BAJETI YA MWAKA WA
FEDHA 2016/2017
Na.Issack Gerald-Katavi
Idara
ya Maji Mkoani Katavi ilisema kuwa mradi wa Orestria unaoshughulikia ukarababti
na ujenzi wa mambomba na vyanzo vya maji unaotarajia kuanza mwezi
ujao,kutawaondolea wananchi adha ya kukosekana kwa maji na hivyo maji
kupatikana kwa saa 24 katika mji wa Mpanda.
Hayo
yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Maji Mkoa wa Katavi Injinia
Zzacharia Nyanda wakati akijibu hoja za wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri
cha kupitisha mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 ambapo kikao hicho
kimefanyika katika ukumbi wa idara ya maji.
Amesema
kuwa mradi huo pamoja na kuweka mabomba mapya ya kupitisha maji,mradi huo
unataraji kujenga chanzo cha Maji Ikorongo Na.2 ili kupata tenki lenye ujazo wa
lita milioni moja huku tenki linguine likjengwa vijijini.
Hata
hivyo Injinia Nyanda amesema kuwa ikiwa mradi wa Oretria hautakuwepo,Shilingi
milioni 7 zitahitajika ili kuondoa
kabisa tatizo la mgao wa maji katika Manispaa ya Mpanda.
Aidha
amesema kuwa tatizo linguine linalopelekea maji kukosekana kwa kiwango kikubwa
katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Katavi hususani Manispaa ya Mpanda ni
kunatokana na kiasi kidogo cha uzalishaji wa maji katika Manispaa ya
Mpanda,mabomba yenye upana mdogo tena ya chuma,mabomba kuziba na mengine
kukatika kutokana na mabomba hayo kuwa ya muda mrefu.
Amesema
kuwa kiwango cha maji kinachozalishwa ni lita mil.3,360,000 huku mahitaji
yakiwa ni lita mil.9,500,000 ambapo kwa kiwango hicho ni sawa na upungufu wa
lita mil.6,140,000.
Bw.Nyanda
alitoa ufafanuzi zaidi wa mradi unaotaraji kuanza mwezi machi mwaka huu.
Baadhi
ya mitaa ya kilimahewa,Kawajense ,Rungwe,Nsemulwa migazini,Aitel na Ilembo
hazina matatizo makubwa ya ukosefu wa maji huku Kata ya Makanyagio na Mpanda
Hotel zikiongoza kwa kuwa na mabomba yaliyoziba mabomba yenye upana mdogo na
kukumbwa na mgao wa maji mara kwa mara.
TAARIFA
YA UFAFANUZI WA MATMIZI YA MITI KATIKA MATUMIZI MBALIMBALI KUPITIA KIKOA CHA
KUPITISHA BAJETI.
Afisa
misitu Wilaya ya Mpanda Bw.Lucas Nyambala alitoa ufafanuzi wa matumizi ya miti
ya kupandwa na isiyo ya kupandwa ambapo miti mingi imekuwa ikitumika kwa
matumizi ya uchanaji mbao,kuni,uchomaji mkaa na matumizi mengine.
Wednesday,
17 February 2016
Posted By:Issack Gerald | At:Wednesday,
February 17, 2016
Na.Agness Mnubi-Nsimbo.
WANAFUNZI
wa Shule za Sekondari katika Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani katavi
wametakiwa kusoma masomo ya sayansi.
Wito
huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Michael Nzyungu wakati
akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA sambamba
na Mpanda redio,akisema kuwa wanafunzi wajitokeze kwa wingi kusoma masomo ya
sayansi ili kufaidi maabara zilizopo katika shule za sekondari za Halmashauri
ya Nsimbo.
Amesema
Lengo la Serikali kujenga maabara kila shule ya sekondari ni kuinua kiwango cha
elimu kwa masomo ya sayansi hivyo wanafunzi hawana budi kusoma masomo ya
sayansi ili kutumia maabara hizo.
Amesema
wanazidi kuboresha maabara hizo kwa kuhakikisha kuwa na miundombinu mizuri, kuongeza vifaa vya kutosha na walimu wa masomo ya
sayansi.
Kauli
ya mkurugenzi mtendaji huyo inakuja ikiwa ni njia mojawapo ya kuhamasisha
wanafunzi kusoma masomo ya sayansi kwa lengo la kupata wataalamu katika masuala
mbalimbali hapa nchini.
Hata
hivyo licha ya hamasa hiyo,kunahitajika walimu zaidi wa masomo ya sayansi wenye
uwezo thabiti.
Thursday, 18 February 2016
AGIZO LA WAZIRI
KUCHUNGUZA MALALAMIKO YA WAKULIMA WA TUMBAKU KATAVI BADO NDOTO,MRAJISI VYAMA
VYA USHIRIKA KATAVI ATOA UFAFANUZI.
Posted By:Issack Gerald | At:Thursday,
February 18, 2016
Na.Issack
Gerald-Katavi
Agizo
la naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi
Mh.Willium Tate Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya ushirika hapa nchini kuteua timu ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa
zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika Mpanda Kati wanaolalamika kutolipwa madai
yao karibu milio 600 halijatekelezwa.
Akizungumza
na Mpanda Radio fm Ofisini kwake,Mrajisi Msaidizi wa Mkoa wa Katavi Bw.Luhiguza
Medadi Sesemukwa amesema kuwa,taarifa iliyopo kutoka kwa mrajisi ngazi ya taifa aliyeagizwa kufanya
ukaguzi huo amesema timu hiyo imechelewa
kufika kutekeleza agizo la waziri kutokana na ukosefu wa fedha.
Bw.Sesemukwa
amesema kuwa,wajumbe wa timu kutoka tume ya maendeleo ya ushirika iliyoundwa na mrajisi wa vyama vya ushirika
nchini inatarajia kufika Mkoani Katavi wakati wowote kuanzia leo.
Hata
hivyo shirika la wakaguzi wa vyama vya ushirika COWASCO kutoka Mkoani Tabora
kwa sasa wapo Mkoani Katavi kuanzia Februari 14 mwaka huu na wanaendelea
ukaguzi wa madai ya wakulima.
Amesema
mara baada ya timu kutoka Dodoma ambako ndiko makao makuu yao yaliko,wataungana
na timu timu iliyotoka Tabora kwa ajili ya kuendelea na ukaguzi na uchunguzi wa
kina.
Agizo
la naibu waziri wa kilimo,mifugo na uvuvi
Mh.Willium Tate Ole Nashe la kumtaka mrajisi vya vyama vya ushirika hapa nchini kuteua timu ya kuchunguza malalamiko ya wakulima wa
zao la tumbaku wa Chama cha Ushirika Mpanda Katavi wanaolalamika kupokonywa
mamilioni hayo ya fedha,lilitolewa Januari 11,mwaka huu akitoka agizo la
kuundwa na kutumwa timu ya ukaguzi ndani ya siku 14 kuanzia siku ya agizo
kutolewa.
Katika
hatua nyingine amewataka wakulima waliotoa hoja ya madai yao kutuo uthibitisho
wa vielelezo ili kubaini ukweli wa malalamiko.
Mbali
na malalamiko ya kutoripwa kitita hicho karibu miloni 600,pia
walilalamikia kulipwa kwa thamani ya
dola badala ya shilingi,kuuziwa pembejeo kwa bei kubwa na kulipa kwa dola na
kutokuona msaada wa Chama kikuu cha ushirika LATCU kwa wakulima wa zao la
tumabku badal aya kuwanyonya.
Wakati
huo huo,amewashauri Mrajisi Sesemukwa ametoa rai kwa wakulima kuendelea kupanda
miti,kutumia Mabani ya kisasa ya kuchomea tumbaku yanayotumia kuni kidogo kwa
ajili ya kuhifadhi mazingira.
Lakini
pia amewataka wakulima kutotorosha tumbaku na kwenda kuuzia nje ya kampuni
iliyoidhinishwa kununua tumbaku yake ili kuepuka kusababisha mlundikano wa
madeni watakayodaiwa.
Majibu
ya mrajisi wa Mkoa,yanakuja kufuatia malalamiko ya wakulima kuanza kujitokeza
wakilalamika kutokuona agizo la waziri kutotekelezeka.
Friday, 19 February 2016
MZIMU WA RUSHWA
WAENDELEA KUWATESA POLISI KATAVI,ASKARI WA JESHI LA POLISI MWINGINE MBARONI
KATAVI KWA KUOMBA NA KUPOKEA RUSHWA
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, February
19, 2016
Na.Issack
Gerald-Katavi
Askari
wa jeshi la polisi Mkoani Katavi PC.G.451 Peter Exavery ameshitakiwa katika
mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya shilingi laki moja
(100,000=/) kutoka kwa mzee aliyefahamika kwa jina la Ruchege Mambalo ili
kumfutia tuhuma ya mkumjeruhi mtoto wake Lutobhisha Mambalo.
Akito
taarifa kwa vyombo vya habari,wakili na mwendesha mashtaka wa Takukuru Mkoani
Katavi Bw.Bahati Stafu Haule,amesema kuwa tukio la askari wa jeshi la polisi
Bw. Peter Exavery Kashuta kushawishi kuomba na kupokea rushwa,lilitokea mnamo
Februari 09 katika Kitongoji cha Lwega kwenye mgahawa wa Lwega,kijiji cha Lwega
Namba 7A,Kata ya Mwese Halmashauri ya
Wilaya ya Mpanda Vijijini.
Bw.
Haule amesema kuwa,Manamo Februari 10,2016,Tume ya kupambana na kuzuia Rushwa
Takukuru Mkoani Katavi lipokea taarifa kutoka kwa Ruchege Mambalo aliyewekwa
mahabusu katika kituo kidogo cha polisi Mwese Februari 09,2016 kwa tuhuma ya
kumpiga mtoto waked Lutobhisha Mbambalo amabaye ana matatizo ya ya akili
alipotaka kumchoma kisu baba yake ambapo katika harakati za kujiokoa,Luchege
mambalo alichukua jiwe na kumpiga mtoto huo usoni ambapo mtoto huyo alikimbilia
haraka kituo cha pilisi Mwese kutoa taarifa.
Amesema
kuwa wakati Bw.Mambalo akimtafuta mtoto wake ali mkuta mtoto huyoakiwa na
askari Peter Exavery Kashuta ambapo baada ya mzazi wa mtoto huyo kufika askari
huyo alishawishi mzee huyo kupewa laki saba (700,000/= ili amwachie huru na
kumfutia tuhuma ya kujeruhi.
Aidha,Bw.
Haule alifafanua kuwa baada ya taratibu za jeshi la polisi kukamilika Februari
17,2016,mtuhumiwa alifikishwa mahakamani katika mahakama ya Wilaya ya Mpanda
mbele ya Mh.Chiganga Tengwa hakimu mfawidhi mkazi wa Wilaya na kufunguliwa kesi
ya jinai Namba.61/02/2016 na kusomewa mashtaka mawili ambayo ni Kuomba au
kushawishi rushwa ya shilingi laki saba(700,000/=) huku shtaka la pili likiwa
ni kupokea rushwa ya shilingi laki moja (100,000) jambo ambalo lilikuwa na
kinyume au matakwa ya mwajiri wake kwa mjibu wa kifungu 15(1)(a) cha sheria ya
kuzuia na kupambana na Rushwa na 11/2007.
Hata
hivyo aliachiwa kwa dhamana ya kukidhi matakwa ya dhamana alizoweka mahakamani
hapo ambazo ni mdhamini mmoja mwenye hati ya au dhamana ya fedha taslimu
milioni bili(2,000.000/=) na kutosafiri nje ya Mkoa wa Katavi bila kibali cha
Mahakama ya Wilaya.
Aidha,Takukuru
Mkoani Katavi imetoa angalizo na wananchi na watumishi wote wa umma kujiepusha
na vitendo vya rushwa huku jeshi la polisi likitakiwa kutambua kulinda usalama
wa raia ikiwa ni pamoja na fedha.
Februari
16 mwaka huu,Mwanasheria Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bw.Falhati Seif Khatibu na
askari magereza wawili wa gereza la mahabusu Mpanda walifikishwa mahakamani kwa
tuhuma za kumtorosha mtuhumiwa wa mauaji ya mlemavu wa ngozi albino.
Kesi
hiyo imepangwa kutajwa tena machi 17 mwaka huu itakaposikilizwa.
RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA
NA WATANZANIA KUPITIA WAZEE WA DAR ES SALAAM HOTUBA YAGUSA MAENEO YOTE.
Rais Dk John Pombe Magufuli Februari 13,2016 alilihutubia
taifa kupitia wa Wazee wa Dar e salaam ambapo ameainisha changamoto kadhaa
zinazolikabili taifa na mikakati inayochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano
kuikabili.
Akizungumza na wazee hao wa Dar es salaam katika ukumbi wa
Diamond Jubilee jijini humo, Rais Dk John Pombe Magufuli amewahakikishia
Watanzania kwamba Serikali ya awamu ya tano anayoingoza imejipanga vyema
kuwatumikia na kukabili matatizo yao.
Katika hotuba yako hiyo iliyochukua takriban saa moja na
kugusa maeneo yote muhimu, Rais ametahadharisha viongozi na wananchi wengine
kuhusu ubadhirifu wa mali ya umma.
Aidha, Rais Dk John Pombe Magufuli amezungumzia kuhusu hali
ya kisiasa visiwani Zanzibar ambapo amesema yeye kama Rais ni vigumu kuingilia
maamuzi ya tume ya taifa uchaguzi Zanzibar ambayo ni huru.
Awali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es saalam alizungumzia changamoto
mbalimbali zinazoukabili mkoa wa Dar es salaa hususan katika utekelezaji wa
agizo la utoaji wa elimu bure.
Katika hatua nyingine,Rais Magufuli aliendelea kusisitiza
kutumbua majipu kwa watu waliokabidhiwa madaraka halafu hawawajibiki ipasavyo
na badala yake kuendekeza ufisadi na kuharibu mali ya umma.
Friday,
19 February 2016
IGP MANGU ATOA
AGIZO KWA MAKAMANDA WA MIKOA YOTE NCHINI KUENDESHA OPARESHENI KALI DHIDI YA
BODABODA.
Posted By:Issack Gerald | At:Friday, February
19, 2016
Na.Mwandihi wetu-Dar es Salaam
Mkuu
wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu amewataka Makamanda wa Polisi kote
nchini kuendesha oparesheni kali ya kuwachukulia hatua kali za kisheria
waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wasiotii sheria za usalama barabarani
ikiwemo kubeba abiria zaidi ya mmoja, kupita katika taa nyekundu pamoja na
kutovaa kofia ngumu.
IGP
Mangu alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Maafisa wakuu wa Polisi wakiwemo
Makamanda wa Polisi wa mikoa, vikosi na makao makuu katika kikao kazi
kilichokuwa kikifanyika jijini Dar es Salaam ambacho kilifunguliwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi.
Alisema
waendesha bodaboda wamekuwa wakikaidi kufuata sheria za usalama barabarani
lakini sasa mwisho wao umefika na kuwataka makamanda wa polisi wa mikoa kote
nchini kutekeleza maelekezo hayo ili kuleta nidhamu kwa bodaboda katika kufuata
sheria za usalama barabarani.
IGP
Mangu alisema suala la kufuata sheria za usalama barabarani kwa bodaboda halina
mjadala na kila kamanda ahakikishe kuwa wale wote wasiofuata sheria na kukaidi
wanakamatwa bila kuoneana muhali kwakuwa wamekuwa wakisababisha ajali
zinazoweza kuzuilika.
“
Pamoja na kuendelea kudhibiti uhalifu wa aina zote, natoa maelekezo kwa
kila mkoa kuhakikisha unaendesha oparesheni kali dhidi ya bodaboda
ili kupunguza ajali zinazosababishwa na bodaboda ambao wengi wao hawataki
kufuata sheria na kanuni za usalama barabarani, tusiwaonee muhali maana maisha
ya watu ni muhimu sana na jambo la msingi ni kusimamia sheria tu” Alisema IGP
Mangu.
Awali
akifungua kikao kazi hicho Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mh. Charles
Kitwanga alilitaka Jeshi la Polisi kuendelea na mapambano yake dhidi ya uhalifu
na wahalifu ili usalama wa raia na mali zao uendelee kuimarika na watanzania
waendelee na shughuli zao za kujiletea maendeleo bila hofu ya kutendewa
uhalifu.
Pamoja
na agizo hilo la IGP Mangu,mwezi uliopita,Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi
Dhahiri Kidavashari akizungumza na na alisema kuwa Oparesheni hili
ilikwishaanza kuanzia mwanzoni mwa mwezi Januari na mafanikio kadhaa
yaliyojitokeza katika opaereheni hiyo ni pamoja na kukamata silaha kadhaa
kutoka kwa wanamiliki silaha kinyume na sheria.
Asante kwa kuendelea kuchagu P5 TANZANIA MEDIA,Mshirikishe na mwenzio
Comments