KUJENGWA MAHAKAMA KATIKA MAKAZI MAPYA YA KATUMBA NA MISHAMO KATAVI KWAPUNGUZA UHARIFU
Na.Issack Gerald-Mpanda
Kujengwa kwa mahakama ya mwanzo katika
eneo la makazi ya Mishamo na Katumba kumepunguza kiwango cha uharifu ambao
umekuwa ujitokeza katika makazi hayo.
Hayo yalibainishwa jana na Wakili wa
UNHCR Adolf Mishanga ambaye ni mkuu wa Ofisi ya UNHCR Mishamo kwa niaba ya Mkuu
wa Ofisi ya UNHCR Wilayani Mpanda katika maadhimisho ya siku ya Sheria duniani
yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya.
Licha ya kutotaja takwimu ya uharifu
katika makazi hayo Bw.Mishanga pia ameiomba idara ya Mahakama kujenga mahakama ya Wilaya katika makazi hayo
ili kurahisha huduma mbalimbali kwa wakazi waliopo katika maeneo hayo.
Wakati huo huo Bw.Misanga alisema
kuwa idadi ya wakimbizi dunia Nzima imefikia milioni 60 huku Mkoani Katavi
idadi ya wakimbizi ikipungua baada ya Tanzania Kutoa uraia kwa waliokuwa
wakimbizi.
Aidha katika kuhakikisha shughuli za
mahakama zinatekelezeka katika kiwango kinachotakiwa,Shirika la Wakimbizi duniani
UNHCR limesema kuwa litaendelea kushirikiana na mahakama Mkoani Katavi na Tanzania
kwa ujumla ambapo katika maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika jana shirika
hilo limetoa nakala 620 vyenye sheria mbalimbali ili kutafsiri sheria namna
ya kuhudumia wakimbizi.
Comments