MAKATIBU WAKUU NA NAIBU KATIBU WAKUU WAAPISHWA,WAZIRI MKUU AWAPONGEZA
Na.Ofisi ya waziri Mkuu.
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewapongeza Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu, mara
baada ya kuapishwa Ikulu leo jijini Dar es Salaam.
Ametoa
pongezi hizo wakati Makatibu Wakuu na Naibu Katibu Wakuu wakiwa wametia saini
hati ya ahadi ya uadilifu kwa viongozi wa umma mbele ya waandishi wa habari.
Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akiongea na Makatibu wakuu na Naibu Katibu wakuu baada ya kusaini Hati ya Maadili ya Umma mara tu baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam leo January 1, 2016 |
Waziri
Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi hao, kuwa waaminifu, kuwajibika na
kutoa taarifa ya utendaji kwa wananchi. Aidha, alisema kuwa, viongozi wengine
watakao apa mbele ya Kamishna wa Tume ya Maadili ni pamoja na Wakuu wa
Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri, ikiwa ni hatua ya Serikali
kudhibiti na kufuatilia matumizi ya rasilimali fedha.
“Wakuu
wa Wilaya watahakikisha fedha zilizoenda katika Halmashauri zao lazima zitumike
katika shughuli zilizokusudiwa” alisema Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu alitoa wito kwa watanzania kuendelea kuwa na imani na Serikali ya Awamu ya
Tano, kwakuwa itatimiza ahadi zote ambazo Mheshimiwa Rais na Makamu wa Rais
walizitoa wakati wa Kampeni.
Makatibu
Wakuu na Naibu Katibu Wakuu hao, wameapishwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John
Magufuli, ambapo shughuli hiyo ilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais Mheshimiwa
Samia Suluhu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Mke wa Mheshimiwa Rais
mama Janeth Magufuli pamoja na viongozi mbalimbali.
Comments