WATAHINIWA 5422 KATI YA 6378 DARASA LA SABA WAFAULU KUJIUNGA NA MASOMO YA SEKONDARI KATAVI 2016
MPANDA-Na.Meshack
Ngumba
JUMLA ya Watahiniwa 5,422 Kati ya watahiniwa 6,378 waliofanya
mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi Mkoani Katavi wamefaulu Kujiunga na Kidato
cha Kwanza Kwa Mwaka 2016.
Akisoma Matokeo hayo jana Katika Kikao cha bodi ya
Uchaguzi wa Wanafunzi watakao jiunga na
Masomo ya Sekondari Afisa elimu Mkoa wa Katavi Bw,Ernest Hinju amesema ufaulu
huo ni sawa na asilimia 85.1
Kutokana na Matokeo hayo Mkoa wa Katavi umeongoza na
kuwa nafasi ya Kwanza Kitaifa Katika
Mikoa iliyofanya Vizuri Katika Mtihani wa Kuhitimu elimu ya Msingi Kwa Mwaka
2015.
Pamoja na Mkoa wa Katavi kushika nafasi hiyo pia Halmasahauri
ya Manispaa ya Mpanda imeendelea Kuongoza Kwa Kuwa nafasi ya Kwanza
Kitaifa kati ya halmashauri zote nchini.
Comments