KIPINDUPINDU KATA YA KAWAJENSE KAMA CHOO HAITAJENGWA
Na.Agness
Mnubi-MPANDA
WAFANYABIASHARA wa soko
la Majengo mapya kata ya Kawajense Manispaa ya Mpanda wanakabilwa na ukosefu wa
huduma ya choo sokoni hapo, hali inayoweza kusababisha magonjwa ya mlipuko kama
vile kipindupindu.
Wakizungumza na Mpanda
radio wafanya biashara hao wamesema tatizo hilo ni la kudumu na uongozi wa Serikali unataarifa juu ya
changamoto hiyo.
Kwa upande wake
Mtendaji wa Kata ya Kawajense John
Salanga amekiri kuwepo kwa changamoto
hiyo kwa zaidi ya miaka mine sasa.
Mtendaji amesema
atahakikisha anajenga choo sokoni hapo kwa kushirikina na wafanyabiashara wa ndani na nje ya soko
na iwapo
utekelezaji huo utashindikana
atafunga soko hilo ili kuepuka magonjwa
ya mlipuko.
Comments