WASAFIRI MPANDA WALALAMIKA TRENI KUTOSAFIRISHA ABIRIA KWA MUDA MWAFAKA
Na.Issack Gerald-MPANDA
Wasafiri wa treni mkoani katavi wamelalamikia suala la kukaa
muda mrefu kwenye kituo cha treni kiasi kinachowafanya kushindwa kusafiri kwa
wakati unaotakiwa.
Malalamiko hayo yametolewa leo na wasafiri wanaotoka wilayani mpanda kuelekea mkoani tabora kuwa
wamekuwa wakiondoka kwa treni muda tofauti na ratiba ilivyopangwa lakini pia kutumia
muda mwingi wawapo safarini.
Wasafiri hao wamekiomba kitengo husika kushughulikia
changamoto zinazo wakabili ili kuondoa usumbufu unaojitokeza.
Kwa upande msimamizi wa kituo cha mpanda bwana Khatibu Nahoda
amesema tatizo kubwa linalosababisha changamoto hizo ni uchakavu wa
mabehewa,uchakavu wa reli pamoja na uchache wa mabehewa hivyo amewataka
wasafiri kuwa na uvumilivu wakati masuala hayo yanashughulikiwa.
Comments