WALEMAVU KATAVI WAOMBA MITAJI NA MIRADI YA MAENDELEO KUONDOKANA NA UMASKINI
Na.Issack Gerald-MPANDA
Watu wenye ulemavu mbalimbali Mkoani Katavi wameiomba
serikali ya Tanzania kuwapatia miradi ya maendeleo pamoja na kujenga miundombinu rafiki kwao
itakayowasaidia kupunguza ugumu wa
maisha.
Hayo yamebainishwa na walemavu hao wakati wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA kuhusu maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.
Baadhi ya walemavu hao ambao wamezungumza na P5 TANZANIA MEDIA ni
pamoja na Katibu wa chama cha walemavu Mkoani Katavi Godfery Sadala na Kalolo
Mses ambao ni waleamavu wa viungo.
Wameuomba uongozi wa Mkoa wa Katavi, kuweka Ofisi itakayokuwa
chini ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda ili walemavu wapate nafasi ya kuonana
na Mkurugenzi na kueleza shida zao.
Maadhimisho ya siku ya Walemavu kitaifa yamefanyika leo
Mkoani Mwanza.
Comments