WANANCHI MKOANI KATAVI WATAKIWA KUCHANGIA DAMU SALAMA
Na.Issack Gerald-MPANDA.
WANANCHI Mkoani Katavi
wametakiwa kujitokeza kwa hiari ili kuchangia damu Salama.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA,Mratibu wa damu
salama Mkoani katavi Henery Silvery
Munah, amesema uratibu wa damu salama kwa Mkoani Katavi ulikuwa ukiratibiwa
Mkoani Rukwa ambapo kuanzia mwezi Octoba mwaka huu wameanzisha zoezi hilo kwa
mujibu wa sheria na taratibu za wizara ya afya na ustawi wa jamii.
Amesema kuna
umhimu mkubwa wa uchangiaji damu kwani zaidi ya chupa 800 za damu salama ambazo hutumika kwa kila
mwezi mwezi Mkoani Katavi.
Aidha ameihakikishia
jamii kuwa damu hiyo inapotumika kwa mgonjwa
hospitalini haiuzwi bali hutolewa bure, na kusisitiza kutoa taarifa
iwapo utauziwa damu.
Comments