BREAKING NEWS : VIONGOZI CHADEMA WILAYANI MPANDA WABWAGA MANYANGA
Na.Issack
Gerald-MPANDA.
BAADHI ya viongozi wa
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilayani Mpanda Mkoani Katavi
wamejiuzuru wadhifa wao kutokana na usaliti
ndani ya chama uliotokea kipindi
cha uchaguzi mkuu wa ubunge urais na madiwani Oktoba 25 mwaka huu.
Wakizungumza na P5 TANZANIA MEDIA katika ofisi za chama
hicho baadhi ya viongozi hao wamesema
wamejihudhuru kutokana na shinikizo la wananchama wa chama hicho kuwataka
wajihudhuru.
Naye mwakilishi wa
wanachama Joseph Mpela ambaye pia alikuwa mgombea udiwani kata ya magamba
amekabidhi barua kwa katibu wa chama kwa niaba ya wananchi inayowataka viongozi
hao kujiuzuru.
Kwa upande wake katibu
wa Chadema Mkoa wa Katavi Almas Ntije amekiri kupokea barua kutoka kwa wananchi
hao na kuomba muda wa kuisoma ili kujua yaliypo katika barua hiyo.
Hata hivyo orodha ya
majina ambao wamejiudhuru yanatarajiwa kuwekwa hadharani muda wowote baada ya
Katibu kutoa tamko
Comments