WANANCHI KATAVI WAPONGEZWA KUENDELEA KUDUMISHA AMANI
Na.Issack
Gerald-MPANDA
Kamanda wa Polisi Mkoani
Katavi Dhahiri Kidavashari,ametoa pongezi kwa wananchi Mkoani Katavi,kwa kuendelea
kudumisha amani katika msimu wa sikukuu za Maulid na Krismasi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi-Dhahiri Kidavashari |
Kamanda kidavashari ametoa
salaamu hizo wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na hali ya
usalama wakati wa sikukuu hizo.
Amesema kuwa,wananchi
Mkoani Katavi wanatakiwa kusherehekea kwa kudumisha amani katika kuuaga mwaka
2015 na kuukaribisha mwaka mpya 2016.
Amesema
ikiwa kila mwananchi atazingatia mwongozo wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977,mkoa wa Katavi utaendelea kuwa salaama wakati wote wa
msimu wa sikukuu za mwaka mpya na baada ya sikukuu hizo.
Hata hivyo Kamanda,ametoa
rai kwa wakazi wote Mkoani Katavi,kuripoti katika jeshi la polisi mapema dalili
zinazoashiria matukio ya uharifu ili yadhibitiwe mapema kabla ya kutokea na
kusababisha madhara.
Asante
kwa kuendelea kunifuatilia katika mtandao huu habari za Katavi na Kwingineko
habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments