ANASWA NA NYARA ZA SERIKALI 38 KATAVI BAADHI NI PUA YA NGURUWE PORI NA KINYESI CHA FISI KWA UNDANI ZAIDI HAPA HAPAP5 TANZANIA
Na.Issack
Gerald-MPANDA
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Vitusi
Chomba(36) mkazi wa Kijiji cha Senkwa Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi
amekamatwa akiwa na nyara mbalimbali za serikali
ikiwemo pua ya nguruwe pori.
Kamanda wa polisi Katavi-Dhahiri Kidavashari |
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Dhahiri
Kidavashari amesema tukio hilo limetokea Mnamo tarehe 27/12/2015 majira ya saa 18:30
katika Kijiji cha Senkwa Tarafa ya Inyonga Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi kwa
ushirikiano na raia wema ambao walitoa taarifa kuhusu vitendo vya mtuhumiwa
kujihusisha na uharibifu wa rasilimali za Taifa.
Kamanda Kidavashari ametaja baadhi ya nyara
ambazo amekamatwa nazo mtuhumiwa kuwa ni pamoja na Vipande 38 vya ngozi ya samba,
Vipande viwili vya ngozi ya panyapori, Mfupa
mmoja wa pundamlia, Gamba mmoja la kakakuona, Mfupa mmoja wa sungura pori, Pua ya
nguruwe pori, Kwato mmoja ya mnyama aina ya muhanga, Mkia mmoja wa sungura, Kipande
cha ini cha mnyama aina ya Insha na kinyesi cha fisi.
Mtuhumiwa anaendelea kushikiliwa na Jeshi la
Polisi kwa hatua za upelelezi na anatarajia kufikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika.
Hata hivyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi
anatoa wito kwa wananchi wanaojihusisha kufanya biashara haramu za magendo kama
vile uharibifu wa rasilimali za Taifa mfano vitendo vya ujangili na uwindaji
haramu kuacha mara moja na wajikite katika kufanya shughuli halali katika
kujipatia kipato vinginevyo hatua kali za kisheria ziaendelea kuchukuliwa dhidi
yao.
Asante
kwa kuendelea kunifuatilia katika mtandao huu habari za Katavi na Kwingineko
habarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments