MKURUGENZI HALMSHAURI YA WILAYA YA KALAMBO,ASIKITISHWA NA HALI YA ELIMU MKOANI RUKWA
Na.Issack Gerald-SUMBAWANGA
MKURUGENZI Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa Bw. Bensoni Kilagi,amesema
hajaridhishwa na matokeo ya darasa la nne na darasa la saba kwa mwaka 2015
mkoani humo.
Akizungumza na P5 TANZANIA MEDIA Kwa njia ya simu,Bw. Kilagi amesema matokeoa yameendelea kuwa mabaya ambapo
kwa mwaka 2014 ufaulu ulikuwa asilimia
thelathini huku mwaka 2015 ufaulu huo ukipanda kwa salimia 10 na kufikia
asilimia 40.
Aidha amesema ili kunusuru hali ya
elimu Mkoani humo,wamekusudia kuitisha vikao vya mara kwa mara vinavyohusisha
wadau wa elimu wakiwemo wazazi,walezi,watendaji na wataalamu wengine wa masuala
ya elimu ili kuongeza kiwango cha ufaulu.
Hata hivyo Bw.Kilangi amezitaja baadhi
ya changamoto zinazopelekea kufanya vibaya katika suala zimala elimu ni kutofanya mazoezi ya mitihani mara kwa
mara ,madawati pamoja na nyumba za walimu.
Comments