MEYA MANISPAA YA MPANDA AOMBA HOSPITALI YA WILAYA YA MPANDA KUHARAKISHWA KUWA MALI YA MANISPAA
Na.Meshack
Ngumba-MPANDA
SERIKALI imeombwa Kuharakisha
Mchakato wa Kuibadilisha hospitali ya Wilaya Kuwa hospitali ya halmashauri ya
Manispaa ya Mpanda ili Kusogeza huduma za afya kwa wakazi wa Manispaa hiyo.
Baadhi ya majengo Hospitali ya Wilaya Mpanda |
Ombi hilo limetolewa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda ambaye pia ni diwani wa Kata ya Majengo Mh,William Philip Mbogo Katika Mahojiano maalum na Mpanda Radio na P5 TANZANIA MEDIA
Katika hatua nyingine Mh Mbogo
ameahidi Kushirikiana na Madiwani wa Kata zote za Manispaa ya Mpanda Kutatua
Kero za wananchi ikiwemo Kusimamia Miradi ya Maendeleo inayoanzishwa Kwa Maslahi
ya wananchi.
Mh,Mbogo anakuwa Meya wa Kwanza wa
Manispaa ya Mpanda Kihistoria tangu halmashauri ya Mpanda ilipopandishwa daraja
Kutoka halmashauri ya Mji mwezi July mwaka huu.
Comments