YATIMA MPANDA WAPATA MSAADA,CHANGAMOTO YA FEDHA HALMSHAURI YA WILAYA YASEMA BADO KIKWAZO KUWASAIDIA YATIMA WENGI
Baadhi ya watoto katika picha ambao wamepatiwa msaada |
NA.Theressia Lwaji-MPANDA KATAVI
WATOTO yatima 12 kati 32 katika kijiji cha ifukutwa kata ya mpanda
ndogo wa halmashauri ya wilaya ya mpanda mkoani katavi wamepatiwa misaada ya magodoro,vyandarua na
blanket.
Akisoma risala kwa
kiongozi wa mbio za mwenge afisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya
mpanda Bahati Mwailapu amesema halmashauri imetoa msaada watoto hao waliofiwa
na wazazi wao ili kujikinga na ugonjwa
wa malaria.
Mwenge wa uhuru Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda |
Aidha Bw.Mwailapu amesema
wanakabiliana na changamoto ya uhaba wa fedha za kuwafikia watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu wilayani
hapa.
Kwa upande wake kiongozi
wa mbio za mwenge kitaifa Juma khatibu chum ameitaka jamii kuacha kutelekeza familia
ili kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Comments