JAMII HALMSHAURI YA WILAYA NSIMBO YATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO KATIKA MALEZI
Baadhi ya viongozi katika Msafara wa mwenge wa Uhuru wakizuru mandari ya Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo wakati mwenge wa uhuru ulipofika katika halmshauri hiyo |
NA.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Jamii katika Halmashauri ya
Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imetakiwa kuwa na
ukaribu kimalezi kwa watoto wao ili
kubaini kwa haraka vitendo vya ukatili wakati vinapotokea kwa watoto.
Wito huo umetolewa na Kaimu Afisa
Maendeleo ya jamii katika halmashauri ya Nsimbo wakati akizungumza na P5 TANZANIA BLOG kuhusu umuhimu wa Wananchi kutoa taarifa za vitendo vya kikatili katika idara
ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri hiyo.
Bw. Mnubi amesema Wazazi na Walezi
kutokuwa na ukaribu kimalezi kwa watoto
wao ni sababu ambayo inachangia jamii kushindwa kugundua kwa haraka vitendo vya
ukatili wakati vinapotokea kwa watoto wao.
Comments