WATOTO KATAVI WATAKIWA KULELEWA MAADILI YA KUITUMIKIA TANZANIA
Waislam katika sgerehe za Eid Elfitri Mjini Mpanda |
Wa nne kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi akishiriki Ibada ya Eid Elfitri Msikiti Mkuu wa Ijumaa Mjini Mpanda |
NA.Issack Gerald-Katavi
Jamii Mkoani Katavi imetakiwa kuwalea
watoto wao katika maadili mema ili kuwatumikia watanzania katika utumishi wa
umma wanapokuwa wakubwa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dr.Ibrahimu Msengi katika sherehe za Idi El Fitri ambazo zimeandaliwa na
Umoja Balaza la Wanafunzi Vijana wa Kiislamu Mkoani Katavi katika viwanja vya
Shule ya Sekondari Istqama iliyopo Mjini Mpanda.
Adha Msengi amewashauri watu wote ndani na nje ya Mkoa wa Katavi waliohitmu
masomo yao na kupata ajira baada ya kusomeshwa na wazazi,walezi ,ndugu ,jamaaa
na Marafiki zao kurejea kuwekumbuka kwa kuwasaidia katika mahitaji wanayoyahitaji.
Katika sherehe hizo ,Mkuu huyo wa
Mkoa ametoa shilingi milioni moja kwa balaza hilo la wanafunzi wa kiislamu kwa ajili
kutumia katika mahitaji ya kuendesha umoja wao.
Sherehe hii pia imehudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa dini ya kiislamu kutoka Dar es Salaam.
Kwa upande wake Shekhe wa balaza la
waislam Mkoa wa Katavi Shekhe Nassoro Kakulukulu amewataka waislamu wote
kuendlea kuitunza na kuienzi amani iliyopo Tanzania bila kujali itikadi za dini
na siasa.
Sherehe za Idd El Fitri ni sherehe ambazo husherehekewa
mara baada ya mfungo mtukufu wa Ramadhani kumalizika
Comments