KATIBU MWENEZI CHADEMA RUKWA NA KATAVI AHAMIA CCM
NA.Issack Gerald-Katavi
Aliyekuwa Katibu mwenezi kupitia
chama cha Demkrasia na Maendeleo Mikoa ya Rukwa na Katavi John Matongo
ametangaza rasmi kujiondoa katika chama hicho na kujiunga na Chama cha
Mpainduzi CCM.
Matongo ametangaza uamuzi huo leo katika
mahoijano maalumu katika studio za Mpanda Radio.
Amesema sababu za kijiondoa katika chama
cha Chadema ni kutokana na ukiritimba na kutoshirkishwa katika vikao na
mikutano ndani na nje ya chama hicho.
John Matongo ambaye pia ni Diwani wa
kata ya Kashaulili anatuhumiwa na chadema kupinga baadhi ya mipango ya
maendeleo ya kukijenga chama.
Katibu huyu ametumikia nafasi ya
uenezi wa chama cha Chadema kwa kipindi cha miaka kumi.
Matongo anakuwa kiongozi wa pili
katika ngazi ya juu wa chadema kutangaza kukihama chama cha Chadema baada ya
Mbunge wa Mpanda Mjini Said Amour Arfi kutangaza kujiondoa katika chama.
Comments