UWT KATAVI WAFANYA UTEUZI WA WAGOMBEA UBUNGE VITI MAALUMU
Na.Issack Gerald-Katavi
MKUTANO Wa umoja wa wanawake wa CCM (UWT)Mkoani Katavi umewateua Taska Restituta Mbogo na Anna
Richad Lupembe kuwa Wagombea wa nafasi
ya Ubunge Vitimaalum kwa Mkoa wa Katavi.
Akisoma Matokeo ya Uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi huo
ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dr Ibrahim Msengi amewataka Wanachama wa Chama hicho Kuepuka makundi ndani ya chama
na badala yake wawaunge Mkono wanachama
walioteuliwa Kuwania nafasi mbalimbali Kuelekea Uchaguzi Mkuu.
Hatua ya kuteuliwa kwa wagombea hao kunakuja ikiwa ni siku
chache baada ya chama cha mapinduzi CCM ngazi ya taifa kumteua John Pombe
Magufuli kugombea kiti cha Urais unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi
Oktoba mwaka huu
Comments