MTOTO ATUPWA NA KUCHOMWA MOTO- KATAVI
NA.Meshack
Ngumba-Mpanda
MTOTO
anayekadiliwa kuwa na umri wa Miezi 6 hadi 7 ametupwa na Kisha kuchomwa
moto Usiku wa Kuamkia Leo Katika Mtaa wa Maridadi Kata ya kashaulili
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi.
Wakizungumza
na Mpanda Fm Katika eneo la tukio wakazi
wa Mtaa huo wameiomba serikali kwa kushirikiana na Jeshi la polisi
Kumtafuta Muhusika na Kumfikisha katika Vyombo vya Sheria ili iwe fundisho
kwa wanawake wengine wenye tabia za Kuwatupa watoto baada ya Kijifungua.
Aidha
wakazi hao wamesema licha ya tukio hilo Kuwa la kwanza kutokea Katika
Mtaa huo Serikali imetakiwa kutolifumbia macho Jambo hilo ili
kunusuru Maisha ya Viumbe visivyo na hatia.
Comments