SAKATA LA WATU KULA VYAKULA WAKIWA KWENYE VYANDARUA,MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA ANG'AKA WAKAZI KUTUPA TAKA SEHEMU ZILIZOZUIWA
Na.Issack Gerald-Katavi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda
Suleiman Lukanga amesema eneo linalolalamikiwa na wakazi wa Mtaa wa Kashaulili
kutumika kama Dampo la kutupa taka na kusababisha Nzi kuzagaa katika makazi yao
lilishapigwa marufuku.
Mkurugenzi huyo anasema hayo leo wakati akizungmza na P5 TANZANIA ikiwa ni
siku mbili baada ya wakazi wa Mtaa wa Kashaulili kusema kuwa wanalazimika kula
chakula wakiwa ndani ya vyandarua kujikinga na nzi wanaozagaa na kuangukia
katika vykula wanapokuwa wanakula.
Aidha Mkurugenzi amesema ikiwa kamati
zinazohusika na usafi katika mtaa huo hazifanyi kazi za kudhibiti utupaji taka
katika eneo hilo watawajibishwa kwa mjibu wa sheria.
Pia amesisitiza kuchukuliwa hatua za
kisheria kwa wakazi wanaotupa taka katika eneo lililozuiwa.
Comments