MWENYEKITI WA MTAA MANISPAA YA MPANDA AZUSHIWA KUJIDHURU,MTUHUMIWA AKANA KUHUSIKA
NA.Issack Gerald-Katavi
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kachoma uliopo
Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Mwarabu Kestokecha amewalalamimkia baadhi ya watu
akiwemo aliyekuwa diwani wa kata ya Makanyagio katika Manispaa hiyo Iddi Nziguye
kwa kusambaza taarifa za kupotosha wananchi kuwa amejiudhuru uenyekiti wa mtaa
huo.
Akizungumza leo na P5
TANZANIA,Kestokecha amesema anasikitishwa kwa uvumi huo unaolenga kuchafua sifa
zake za uongozi.
Kestokecha ambaye ni mwenyekiti
kupitia chama cha CHADEMA amewataka wakazi anaowaongoza kutofuata maneno
yasemwqayo mitaani na kusema kuwa anatambua thamani ya kura yao hivyo hawezi kutupa
thamani ya kura waliyompa.
P5 TANZANIA imemtafuta mmoja wa
watuhumiwa Idd Nziguye ambaye hata hiyo amekana kuhusika na usambazaji wa uvumi
huo wa mwenyekiti huyo kujidhuru.
Mwarabu na Nziguye wote walilkuwa
chama kimoja cha Chadema isipokuwa Nziguye inasemekana amehamia Chama kipya cha
ACT Wazalendo kilichopo chini ya
kiongozi Zitto Zubery Kabwe
Comments