MKUU WA MKOA WA KATAVI AFUTURISHA,MAMIA KADA MBALIMBALI ALIOWAARIKA WAHUDHURIA AWAASA KUDUMISHA AMANI
Mkuu wa Mkoa akizungumza na kada mbalimbali aliowaarika kushiriki kwa pamoja katika Ikulu ndogo Mjini Mpanda |
Mkuu wa Mkoa katikakti wakifuturu |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi wa NNE kutoka kulia katika picha wakiswali |
Na.Issack Gerald-Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Dk. Ibrahim Hamisi Msengi
amesisitiza kuwepo kwa amani, upendo na ushirikiano na kusema kuwa ni fursa nzuri kwa watu kufanya shughuli za
maendeleo.
Dk. Msengi ametoa kauli hiyo jana katika hafla
fupi ya kufuturisha iliyofanyika Ikulu ndogo mjini Mpanda.
Aidha amewataka wakazi wa mkoa wa Katavi
kuondoa tofauti za itikadi za kidini na kisiasa na badala yake amewataka
kudumisha amani.
Amesema kuwa kuepukana na vitendo viovu
kutadumisha umoja wa watanzania kama ilivyo sasa ambapo Watanzania wote ni
wamoja na wanashirikiana kwa kila jambo.
Akizungumzia dalili za uovu,Mkuu huyo wa Mkoa
amewataka wakazi wote mkoani Katavi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pindi
wanapoona kuna dalili zozote za uvunjifu wa amani ili hatua za haraka
zichukuliwe.
Hafla hiyo fupi ya futari, ilihudhuriwa na viongozi
wa dini wakiongozwa na askofu wa kanisa la New harvest Afrika mashariki na kati
Askofu Laban Ndimubenya, viongozi wa serikali, waumini wa dini mbali mbali na
waandishi wa habari.
Comments