MIL.40 KUOKOA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI IGALULA WANAOSOMEA NJE WILAYANI MPANDA
Wanafunzi Shule ya Msibgi Igalula chini ya Mti wakitumia mti huo kama darasa |
Juma Khatibu Chum akizindua vyumba vya madarasa Shule ya Msini Igalula ilyopo Wilayani Mpanda |
Wanafunzi wa Chekechea Igalula Wilayani Mpanda wakiwa darasani |
NA.Theressia Lwanji- Katavi
Ujenzi
wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Igalula unatarajia
kupunguza adha ya uhaba wa madarasa katika shule hiyo na kuondoa adha hiyo
inayowapata wanafunzi shuleni hapo.
Kujengwa
kwa madarasa hayo kunapunguza idadi ya vyumba vya madarasa kwa shule za msingi
wilayani mpanda mkoani katavi.
Akisoma
taarifa ya ujenzi wa vyumba hivyo kwa kiongonzi wa mbio za mwenge kitaifa
mwalimu wa shule hiyo Brown Jasson amesema ujenzi huo utakuwa na manufaa kwa
wananchi kuwapeleka watoto shule ili
kupata haki yao ya msingi.
Amesema
halmashauri imewashirikisha wananchi katika ujenzi huo ili kutekeleza ilani ya
serikali ya kuwashirikisha wananachi ili kutambua kuwa miradi ni yao.
Aidha
amesema mradi huo umegharimu shilingi milioni arobaini na nne mia tisa elfu ambazo ni mchango wa
halmashauri,shilingi milioni therathini mia nne elfu kutoka kwa wahisani, milioni
kumi na moja kutoka chama cha msingi cha tumbaku na nguvu za wananchi zikipatikana
milioni tatu na laki tano.
Comments