JESHI LA POLISI KATAVI LAWAONYA WATAKAOSABABISHA UVUNJFU WA AMANI SHEREHE ZA EID EL FITR
Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi Dhahir Athman Kidavashari akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) akizungumzia suala la kudumisha amani Mkoani Katavi |
JESHI La Polisi Mkoani
Katavi limetoa tahadhari kwa watu kutojihusisha na Vitendo vya Uvunjifu wa
amani wakati wa Sherehe za Eid el Fitr inayoadhimishwa leo hapa nchini Tanzania.
Taarifa ya Jeshi la Polisi
Mkoani hapa kwa vyombo vya habari imesema
Uzoefu unaonesha kuwa kipindi cha Sherehe kama hizi hukumbwa na Matukio
mbalimbali na hivyo kuwataka wananchi kuwa Makini na Kuchukua tahadhari ya
Kuhakikisha usalama wa nyumba zao.
Miongoni mwa matukio
ambayo hujitokeza nyakati kama hizi ni Wizi,ulevi wa Kupindukia na Ubakaji
ambapo Jeshi la polisi limejipanga Kukabiliana na Mtu au Kikundi kitakacho
husika Kuvunja Sheria ya Nchi.
Comments