USALAMA KAMBI YA WAKIMBIZI KATUMBA RAIA WAPYA TANZANIA YAENDELEA KUIMARIKA
HALI YA USALAMA imeendelea kuimarishwa zaidi katika kambi ya wakimbizi
ya Katumba iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.
Hayo yameelezwa leo na Inspector Msaidizi wa Polisi katika
kambi hiyo NDITA MALE Katika mahoijiano
na mwaandishi wa habari wa blogi hii katika
kambi hiyo.
Katika hatua nyingine Insipecta Male amekanusha taarifa za
Uvumi wa kuwa jamii ya Watanzania wapya wanajihusisha na Vitendo vya Uhalifu
katika maeneo mbalimbali Mkoani Katavi na kuongeza kuwa Uhalifu uliokuwa ukijitokeza
kipindi cha Nyuma kwa sasa umedhibitiwa.
Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo wakazi Katika kambi hiyo wametakiwa kuachana na
Vitendo vya uhalifu wa aina yoyote ili kuepuka Mkono wa Sheria.
Zoezi la kutoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi walioishi zaidi ya miaka arobaini nchini
Tanzania wengi wao wakitokea nchini Burundi lilifanyika mwaka jana ambapo
wakimbizi zaidi ya laki moja walipewa uraia.
Mkoa wa Katavi una makambi mawili ya wakimbizi ambayo ni
Katumba yenyewe iliyopo halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo na Kambi ya mishambo
iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
Comments