BALAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MKOANI KATAVI LAVUNJWA
Na.Issack Gerald-Nsimbo,Katavi
BARAZA la Madiwani Katika halmashauri
ya Nsimbo Mkoani Katavi limevunjwa jana kwa Mjibu wa kanuni za baraza hilo ambalo
humaliza muda wake wa kuwa madarakani
Kila baada ya Kipindi cha Miaka mitano.
AKizungumza katika kikao cha mwisho
cha baraza hilo mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo Mohamed Asenga amesema kwa kipindi cha Miaka mitano Madiwani
kwa kushirikiana na watalaam wamefanya kazi kubwa ya Kuleta maendeleo Katika
jamii licha ya Halmashauri ya Nsimbo kuwa changa.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Mlele Kanali ISSA SULEIMAN NJIKU mbali na kutoa pongezi kwa madiwani wote kwa
kufanikisha shughuli za maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano,amewataka
madiwani watakaochaguliwa katika Uchaguzi Ujao wa urais ubunge na udiwani kuendeleza
Ushirikiano wa kuleta maendeleo ya wananchi.
Halmashauri ya Wilaya nsimbo
imetokana na Halmashauri ya Mpanda vijijini, ambapo imevunja baraza la madiwani kwa mara ya kwanza ikiwa na madiwani kumi na
nne.
Miongoni mwa miradi ya maendeleo
ambayo imeshughulikwa katika kipindi cha miaka mitano ni miradi ya maji,ujenzi
wa jengo la Halmashauri ya Wilaya na ujenzi wa maambara katika shule za
sekondari.
Halmashauri hii ni miongoni mwa
halmshauri nne zilizopo Mkoani Katavi ambazo ni Halmashauri za Mpanda
Mji,Mpanda Vijijini,Nsimbo na Mlele.
Comments