WAZIRI WA MAJI ISACK KAMWELWE ATEMBELEA BWAWA LA IGOMBE TABORA ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Waziri wa Maji na
Umwagiliaji,Mhandisi ISACK KAMWELWE amewataka wananchi Mkoani Tabora kutoharibu
mazingira ya bwawa la Igombe ambalo kwa sasa limejaa ili kuzuia upotevu wa maji
unaosababisha kero ya mgao wa maji.
Waziri Kamwelwe ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Katavi Mkoani Katavi,ametoa rai hiyo alipotembelea
bwawa la Igombe kukagua hali ya ujazo wa maji ambapo amesema wananchi wamekuwa
wakilima pembezoni mwa bwawa hilo na kusababisha upotevu wa maji hivyo ni vyema
wakaacha utamaduni huo.
Amesema ili kuhakikisha wakazi wa Tabora
wanaendelea kupata maji,serikali inaendelea kutekeleza mradi wa maji kutoka Ziwa
Victoria ambapo kwa sasa tayari mabomba ya kupitishia maji tayari yameanza
kufika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji
wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Tabora-Tuwasa Mhandisi Mkama
Bwire amesema ujazo wa maji katika bwawa la Igombe umeongezeka kutoka mita moja
mwaka jana hadi kufikia mita 4.6 kwa sasa hali ambayo imeondoa adha ya mgao wa
maji.
Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora,Mwalimu
Queen Mlozi amempongeza Waziri Kamwelwe kwa juhudi zake za kuhakikisha
changamoto ya mgao wa maji inaondoka kwa wakazi wa Tabora.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa
Tuwasa,Mhandisi Mkama Bwire mwaka jana mamlaka hiyo ilikuwa ikitumia zaidi ya
shilingi milioni 200 kila mwezi kutibu maji lakini kwa sasa kiwango hicho
kimepungua hadi kufikia milioni 180 na kinatarajia kupungua zaidi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments