MBUNGE WA KATAVI AMETETEA WANANCHI WALIOPO KATIKA MIPAKA YA HIFADHI YA RELI,WAKAZI WA MTAA WA MSASANI,TAMBUKARELI NA ILEMBO WAMEGUSWA
Na.Issack Gerald
SERIKALI imesema haina
Mpango wa kulipa fidia kwa wakazi waliovamia hifadhi ya reli katika kipindi cha
miaka ya 1904.
Mh.Roda Kunchela(Chadema) |
Akiuliza swali bungeni
mjini Dodoma,Mh.Roda Kunchela mbunge wa viti maalumu mkoani Katavi,amehoji mkakati
wa serikali uliopo kwa sasa kuwalipa fidia wakazi wa mitaa ya Msasani,Tambukareli
na Ilembo watakaobomolewa makazi ya hivi karibuni.
Akijibu swali hilo,Naibu
Waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Atashasta Justus Nditiye
pamoja na mambo mengine amesema watakaolipwa fidia ni wakazi watakaokutwa na
reli katika maeneo yao.
Katika hatua nyingine,Naibu
Waziri Mhandisi Atashasta Justus Nditiye amesema serikali itawachukulia hatua
watumishi wote waliopimi viwanja hifadhi ya reli na kuwaruhusu wananchi
kujenga.
Wakazi wa mitaa ya
Tambukareli na msasani wanatakiwa kupisha maeneo ya hifadhi ya reli kabla ya
Mwezi Januari mwaka 2018.
Serikali ya awamu ya
tano imedhamiria kujenga mtandao wa reli ya kati katika kiwango cha kimtaifa cha
Standard Gauge yenye urefu wa kilomita 4886 ambapo katika ukanda wa kati ni urefu
wa 2561 ikiwa ni kutoka Dar-Isaka-Mwanza,Tabora-uvinza-Kigoma kilomita 411,Kaliua-
Mpanda-Karema kilomita 321,Isaka-Rusumo kilomita 371 wakati kilomita 36 ni
kutoka Keza-Ruvubu na Uvinza- Kalelema-Msongati kilomita 203.
Ukanda wa Kusini
unaojumuisha reli kutoka Mtwara hadi Mbambabay yenye matawi yake ya kuelekea
Liganga kwa ajili ya chuma na Mchuchuma kwa ajili ya makaa ya mawe ina urefu wa
kilomita 1092 huku ukanda wa Kaskazini unaojumuisha mikoa ya Tanga,Arusha hadi
Musoma ikiwa na urefu wa kilomita 1233.
Kikao cha leo ni cha kwanza katika bunge la 11 katika mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Kikao cha leo ni cha kwanza katika bunge la 11 katika mkutano wa tisa wa bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED
Comments