MH.SAMIA SULUHU HASSANI AONYA MATUMIZI YA KAMERA NA TOCHI KUTOKUWA CHANZO CHA UCHUKI KATI YA SERIKALI NA WANANCHI
NA.Issack Gerald-Moshi Kilimanjaro
MAKAMU wa rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan amewataka askari wa usalama
barabarani kutotumia kamera na tochi kuwanyanyasa wananchi hali inayochochea
chuki kati ya serikali na wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassani wakati
akizindua wiki ya Nenda kwa usalama uzinduzi ambao umefanyika Wilayani Moshi
Mkoani Kilimanjaro.
Aidha Makamu wa rais Mh.Samia Suluhu
hasani ameliagiza baraza la usalama barabarani kuhakikisha kila anayeendesha
chombo cha moto awe na leseni halali huku wamiliki wa mabasi kwa upande wao
wakitakiwa kuwa sehemu ya kuzua ajali hapa nchini.
Kwa upande wake baraza la usalama
barabarani hapa nchini limesema maadhimisho ya wiki ya nenda klwa usalama
barabarani ni sehemu ya mkakati endelevu unaowaelimisha na kuwakumbusha
madereva na watumia barabara wote nchini kutambua wajibu wao wawapo barabarani.
Aidha Baraza limesema mpango wa
kupambana na ajali hapa nchini kumesaidia kupunguza ajali kwa asilimia 49
katika kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu.
Kauli mbiyu katika wiki ya nenda kwa
usalama mwaka huu ni ‘’Zuia Ajali,Tii
sheria Okoa Maisha’’.
Comments