HALMASHAURI YA WILAYA NSIMBO MKOANI KATAVI WANAFUNZI 14 WAPATA UJAUZITO
Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Moja ya picha ya wanafunzi Mkoani Katavi |
Afisa ustawi wa jamii katika
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Bi.Dianarose Mnuo amesema miongoni mwa mambo
yanayochangia wanafunzi kupata mimba wakiwa mashuleni ni kutokuwa na mabweni,wazazi
kutowalinda watoto,umbali anakotoka mwanafunzi pamoja na umaskini.
Amesema kati ya wanafunzi hao
14,wanafunzi watano wanatoka shule ya msingi Ugalla,Katumba na Kanoge huku 9
waliopo katika Shule za sekondari wakitoka shule za sekondari Katumba yenye
wanafunzi 3,Sule ya Sekondari Nsimbo wanafunzi 5 na sitalike 1.
Hata hivyo amesema kumekuwa na
changamoto ya wasichana wanaopewa ujauzito kuwataja wahusika wanaowapa mimba
pamoja na wahusika wa pande mbili kupeana rushwa ili kumaliza tatizo wao
wenyewe kwa wenyewe.
Katika kukabiliana na baadhi ya
changamoto,Halmashauri imekusudia kujenga mabweni ya wasichana ikiwemo katika
shule ya Sekonadri Nsimbo ambapo wapo katika mchakato.
Kwa mjibu wa Afisa Ustawi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Kesi zote 14 zimeripotiwa katika vyombo vya
sheria ambapo hata hivyo hakuna ripoti inayoonesha kutolewa adhabu kali kwa
wanaowapa mimba wanafunzi Mkoani Katavi.
Kutokana na Mkoa wa Katavi kuongoza
kwa asilimia 45 katika mimba za utotoni,mkoa wa Katavi unatarajia kufanya
maadhimisho hayo kimkoa katika Manispaa ya Mpandahuku ikitanguliwa na kongamano
litakalofanyika leo ili kujadili matatizo ya mtoto wa kike ikiwa ni kuelekea kilele cha maadhimisho ya
siku kike Duniani kitaifa yakiadhimishwa Mkoani Mara.
Katika maadhimisho hayo
yanayoadhimishwa Oktoba 11 ya kila mwaka,Kaulimbiyu kwa mwaka huu inasema’’Siku ya kimataifa ya mtoto wa
kike,tokomeza mimba za utotoni tufikie uchumi wa viwanda’’
Habari zaidi ni www.p5tanzania.blogspot.com
au ukurasa P5Tanzania Limited au P5Tanzania Limited Group
Comments