VIJANA UVCCM MKOANI KATAVI WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU SALAMA HOSIPTALI YA WILAYA YA MPANDA
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mpanda
Katavi
VIJANA WA UMOJA wa chama cha
Mapinduzi UVCCM Mkoani Katavi,leo wamejitokeza kuchangia damu salama katika
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.
Katibu wa umoja wa vijana UVCCM
Mkoani Katavi Bw.Shua Masanguti amesema vijana wa chama hicho wapatao 80
wakiwemo wanawake 8 wamaejiotokeza kuchangia damu salama ili kunusuru maisha ya
wagonjwa wanaolazimika kuongezewa damu.
Aidha Bw Masanguti amesema wamechukua
hatua hiyo baada ya kutambua kuwa kuna uhitaji mkubwa wa damu kwa wagonjwa
katika ikiwa pia ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana duniani ambayo kilele
chake ni Oktoba 14 mwaka huu.
Mmoja wa wataalamu wa idara ya
kitengo cha damu salama katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Rinus Zenobi
Kawana mbali nakuwapongeza chama cha
Mapinduzi CCM kwa uamuzi wa kutoa damu salama kwa ajili ya wagonjwa pia ametoa
wito kwa makundi mengine kuendelea kujitokeza ili kuchangia damu.
Katika hatua nyingine Muuguzi Mkuu wa
Manispaa ya Mpanda Dkt.Alexanda Gervas Kasagula
mbali na kuwapongeza vijana wa CCM kwa kujitokeza kuchangia damu salama
amesema,ujenzi wa duka la kuhifadhiwa dawa linalojengwa na Bohari ya dawa hapa
nchini MSD katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda limefikia hatua nzuri licha ya kuwa
hata hivyo linaonekana kuwa dogo ukilinganisha na kiasi cha dawa kinachohitajika
kuhifadhiwa katika duka hilo.
Ujenzi wa duka ni utekelezaji wa
Agizo la Wziri Mkuu aliyeagiza kujengwa maduka ya madawa katika Hospitali zote
hapa nchini ili kutatua tatizo la ukosefu au uhaba wa dawa kwa ajili ya
wagonjwa.
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo
zamani ilikuwa ikimilikiwa na Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda kabla ya Manispaa
ya Mpanda kukabidhiwa hospitali hiyo,bado ina uhaba wa damu kwa ajili ya
wagonjwa wenye uhitaji wa kuongezewa damu.
Comments