MKUU WA MKOA WA KATAVI APOKEA SHILINGI 500,000/= KUTOKA MUKABUBINGA KWA AJILI WAATHIRIKA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA,FEDHA ILIYOCHANGWA YAFIKIA MIL. 13,344,600 KUWASILISHWA KAGERA JUMATATU.
Na.Issack Gerald Bathromeo - Katavi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald) |
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald) |
Mmoja wa viongozi wa umoja huo Bw.Rugalema
Gelasius akiwasilisha taarifa kwa niaba ya umoja huo,amesema walipokea kwa
masikitiko makubwa ya tukio la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu
17,majeruhi na kusababisha uharibifu wa mali,makazi ya watu,shule na vituo vya
huduma za afya.
MUKABUBINGA ni
neno ambalo limeundwa na Wilaya za Muleba,Karagwe,Bukoba,Biharamulo na Ngara
zote za Mkoa wa Kagera.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga mbali na kuupongeza umoja wa
wanakagera hao,amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 13,344,600 zimekwishapatikana
ili kuwasaidia waathiriwa ambapo fedha hiyo inatarajiwa kuwasilishwa Mkoani
Kagera Jumatatu Ijayo ya Oktoba 10,2016.
Wakati huo huo wana umoja wengine wa MUKABUBINGA
wanaotoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kagera mbali na kueleza na tetemeko
hilo,wameziomba taasisi nyingine na mtu mmoja mmoja kujitokeza kuwachangia
walioathirika.
Umoja wa wanakagera waishio Mpanda
MUKABUBINGA wapatao 29 walioanzisha umoja huo mwaka 2002,wamekabidhi fedha hiyo
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi
sambamba na waandishi wa habari Mkoani Katavi.
Tukio la tetemeko la ardhi lilitokea
Septemba 10 mwaka huu ambapo pia mbali na kuathiri upande wa Tanzania,pia nchi
zikiwemo Uganda na Kenya ziliguswa na tukio hilo.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments