JIMBO LA MPANDA MJINI LAPATA MGAO WA MADAWATI 537 KUTOKA MFUKO WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda
JIMBO la Mpanda mjini Mkoani Katavi
limepatiwa mgao wa madawati 537 kutoka mfuko wa ofisi ya bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Hayo yamebainishwa jana Oktoba 14na
Mbunge wa Jimbo hilo Mh.Sebastian Simon Kapufi wakati akihututubia wakazi wa
kata ya Mpanda Hotel katika mkutano wa hadahara.
Amesema kuwa mara baada ya kuletwa madawati
hayo ambayo kwa sasa yapo Sumbawanga Rukwa mara baada ya kuwasiliwhwa Jimboni yatagawiwa
kwa shule zenye upungufu wa madawati.
Katika hatua nyingine Mbunge
Mh.Kapufi ametoa msaada wa Zaidi ya shilingi milioni mbili kwa makundi tofauti
yaliyopo Kata ya Mpanda Hotel.
Misaada hiyo ambayo imetolewa na
Mbunge ni pamoja na Shilingi Milioni 1 kwa ajili ya ukarababti mabomba ya maji
Mpanda Hotel huku fedha nyingine ikitotolewa kwa makundi ya wapepeta pumba za
mchele waliopatiwa Shilingi 500,000/=,na wagonwa wengine ambao wamepatiwa fedha
taslimu kuanzia shilingi elfu kumi na tatu hadi laki mbili(13,000/= hadi
200,000/=.
Wakati huo huo huo suala la tatizo la
maji,umeme na migogoro ya ardhi imetajwa na wananchi kuwa kikwacho cha
maendeleo ya wananchi.
Hata hivyo juzi Oktoba 13,2016 katika
kikao cha baraza la madiwani Manispaa ya Mpanda kulijadiliwa mikakati
inayofanyika namna ya kutatua matatizo ya maji,umeme na migogoro ya ardhi
katika Maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Mpanda.
Jimbo la Mpanda Mjini lina Jumla ya
kata zipatazo 15.
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments