GEREZA LA KALILANKULUKULU NA TAASISI ZAKE AMBAZO NI SHULE NA ZAHANATI HATARINI,BAADHI YA WAFUNGWA HAWANA SARE,BAADHI YA ASKARI MAGEREZA NAO WALAZIMIKA KUTUMIA PESA ZAO KUSHONA SARE KWA MIAKA 8 SASA,KUTA ZA MAJENGO YA ZAHANATI NAYO KUANGUKA MUDA WOWOTE,VYOO VYA WANAFUNZI NAVYO VYAJAA VYAZIBA BILA HATUA KUCHUKULIWA KIPINDUPINDU KUBISHA HODI.
Na.Issack Gerald Bathromeo
Mashama-Tanganyika Katavi
GEREZA la Kalilankulukulu lililopo
Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi lililoanzishwa mwaka 1973 ,linakabiliwa na matatizo
mbalimbali yakiwemo baadhi ya wafungwa wa gereza hilo kukosa sare huku pia baadhi
ya asakari wa gereza hilo,wakilazimika kutumia pesa yao kushona sare zao
kutokana na serikali kutowapa sare hizo tangu mwaka 2009 licha ya viongozi
kadhaa wa wizara,Mkoa hadi Wilaya kuwa na taarifa ya matatizo hayo.
Mwigulu Nchemba waziri wa mambo ya ndani ya Nchi ambaye kwa kiasi kikubwa gereza zipo chini ya wizara yake kama waziri |
Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe Naibu waziri wa Nishati na madini(Mbunge wa Jimbo la Katavi) |
Hali hiyo ya kukosekana kwa sare za
wafungwa imethibitishwa na Mkuu wa Gereza la Kalilankulukulu ACP Samwel Oberthe katika ziara ya kushtukiza ambayo imefanywa
leo na mbunge wa viti maalumu Mkoani Katavi
Taska Mbogo,katika ziara ambayo alikuwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Saleh Mhando huku tatizo la askari magereza kutumia pesa yao
likithibitishwa na baadhi ya askari magereza ambao hawakutaka majina yao
yatajwe.
Aidha Katika ziara hiyo,Mkuu wa
Gereza la Kalilankulukulu ACP Samwel Oberth amezitaja changamoto nyingine
zinazolikabili gereza hilo kuwa ni ukosefu wa umeme,maji ambapo wafungwa
hualzimika kuchota maji tena yasiyo salama katika maenewo ya kona Mnyagala
umbali wa kilomita 8 huku changamoto nyingine ya gereza hilo ikiwa ni hali
mbaya uchakavu wa majengo ya gereza hilo.
Wakati huo huo ACP Oberthe amesema majengo
ya zahanati ya Kalilankulukulu yapo hatarini kuanguka kutokana na kuwa na nyufa
kubwa za muda mrefu ambapo huenda muda wowote kukatokea madhara makubwa kwa
watumiaji wa majengo ya zahanati hiyo.
Nao baadhi ya wafungwa wakizungumza
mbele ya mbunge wameeleza kusikitishwa na kutopata nakala za hukumu zao kwa
muda mrefu na kutopata mrejesho wa rufaa wanazokuwa wamekata ambapo Mkuu wa
Wilaya kwa kushirikiana na Mkuu wa Gereza wameahidi kufuatulia ili wafungwa
wapate majibu yao kwa mjibu wa sheria.
Katika hatua nyingine Mwalimu Mkuu wa
shule ya Msingi Kalilankulukulu Boazi Masoko,akizungumza katika ziara ya mbunge
huyo amesema,matundu ya vyoo 5 vya shule hiyo yanayotumiwa na wanafunzi wapatao
500 yamejaa na kuziba tangu mwaka jana,ambapo hali hiyo inatishia muda wowote kutokea milipuko wa magonjwa ya kipindupindu ikiwa serikali
na wadau hawatachukua hatua za haraka kunusuru hali hiyo.
Kwa mjibu wa taarifa ya mkuu wa
Gereza,kwa mwaka 2016 miongoni mwa viongozi waliopata na taarifa ya changamoto
za gereza hilo ikiwemo baadhi ya
wafungwa kutokuwa na sare ni Pamoja na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi
Mh.Mwigulu Nchemba ambaye alipata taarifa alipofanya ziara Mkoani Katavi mwaka
huu,huku changamoto ya ukosefu umeme akipewa naibu waziri wa nishati na Madini.
Katika changamoto ya Ukosefu wa maji,wizara
ilipata taarifa kupitia kwa naibu waziri wa maji na umwagiliaji Mhe. Mhandisi
Isack Kamwelwe (Mbunge Jimbo la Katavi) ambapo viongozi wote kwa pamoja kwa
nyakati tofauti waliahidi kuzifanyika kazi.
Hata hivyo,agizo la kupelekwa umeme
katika gereza la Kalilankulukulu alilolitoa naibu waziri wa nishati na Madini
kwa mwezi Agosti mwaka huu kwa Shirika na umeme Tanzania TANESCO Mkoani Katavi
,halijatekelezwa licha ya shirika hilo kusikika kupitia vikao mbalimbali
likitoa taarifa ya mkakati wa umeme Mkoani Katavi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya
Tanganyika Saleh Mhando amesema lazima matatizo ya gereza hilo hususani
zilizopo chini Wilaya yake hatua za ufumbuzi zianshwe ambapo kwa Upande wake
Mbunge Taska Mbogo mbali na kuahidi kuwasilisha matatizo ya wafungwa wa gereza
hilo Bungeni pia ametoa msaada wa Zaidi ya laki tatu kwa ajili ya kununua
vyombo kwa ajili ya kulia vyakula ambapo tatizo hilo nalo limekuwepo kutokana
na kuongezeka kwa wafungwa kutoka 45 miaka iliyopita hadi 176 kwa sasa.
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa
maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
Comments