MIFUGO KUZAGAA MITAANI KWAPIGWA WILAYANI KIBONDO
Na.Mwandishi wetu- Jastini
Cosmas-Kibondo Kigoma
HALMASHAURI ya wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma,imewaagiza
wananchi katika Halmshauri hiyo kutoachia mifugo yao ovyo katika kipindi hiki
cha msimu wa kilimo,kutokana na mifugo hiyo kuwa waharibifu wa mazao.
Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Kibondo
Bw.Simoni Kanguye katika kikao cha baraza la madiwani wa halmshauri.
Aidha Kanguye,amewataka watendaji wa kata kuhakikisha kila mfugaji
anaidhibiti mifugo yake ipasavyo.
Wakati huo huo Bw.Kanguye ameongeza kwa kusema kuwa atakayebainika kuachia mifugo ovyo
na kusababisha kuharibu mazao, atachuhukuliwa hatua kali za kisheria ikiambatana
na faini.
Katika kutekelezwa kwa agizo hilo,maafisa watendaji wa Kata
na Vijiji wameagizwa kusimamia zoezi la kutozagaa kwa mifugo ya wananchi na
kuhakikisha wananchi wanazingatia maagizo ya Halmashauri.
Pata
habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments