KINACHOIGUSA MIKOA YA KATAVI,RUKWA NA KIGOMA KUTOKA VIKAO VYA BUNGENI DODOMA LEO SEPTEMBA 8,2016
Na.Issack Gerald-Dodoma
Serikali
imesema,inaendelea kuweka mikakati ya kuwa na kiwanda cha kutengeneza pikipiki
za bodaboda ili kuwajengea vijana kuwa na uwezo wa kununua pikipiki zao,kuliko
kuendelea kuwatumikia matajiri wenye uwezo wa kumiliki pikipiki hizo.
Wabunge wakiwa bungeni Mjini Dodoma leo Septemba 8,2016 |
Kauli hiyo
imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki
Mh.Suzan Kolimba wakati akijibu swali la Mh.Munde Tambwe mbunge viti maalumu
Tabora aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali kuwekeza katika ujenzi wa
viwanda vya kutengeneza pikipiki hapa nchini ukiwemo mkoa wa Tabora.
Mh.Tambwe
amesema,ikiwa kiwanda cha Bodaboda kitajengwa Mkoani Tabora,vijana walio mikoa
jiarani kama Katavi,Rukwa na Kigoma watanufaika kwa ukaribu zaidi.
Katika
hatua nyingine Mh.Kolimba amesema,Wizara imekwishafanya mikakati ambapo na
inaendelea v majadiliano na serikali ya chinayanaendelea kuhakikisha Serikali
ya China inawekeza katika kilimo cha Tumbaku ili mku;lima wa Tanzania anufaike
na zao la tumbaku.
Comments