WATENDAJI WA HALMASHAURI MKOANI KATAVI WATAKAOCHEZEA FEDHA ZA MAENDELEO KUUNGUZWA
Na.Issack
Gerald Bathromeo-Mpanda
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka
watendaji wa halmashauri mkoani Katavi kuwa makini na matumizi ya fedha za
maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao na atakayethubutu kuzichezea
zitamuunguza.
Waziri Mkuu akiwapungi amkono wananchi |
“Fedha hii tafadhali ni ya moto. Msicheze
na hii ya halmashauri tunayoileta hapa halmashauri kwa ajili ya wananchi
itawakunguza vidole. Tunaileta kwa madhumini, tunataka wananchi wahudumiwe,“
alisema.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana jioni wakati akihutubia umati mkubwa wa wananchi kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika kiwanja cha Azimio wilayani Mpanda.
Alisema Serikali imeanza kupeleka fedha za miradi ya maendeleo
katika halmashauri mbalimbali hivyo ni vema kila mtendaji ahakikishe fedha hizo
zinatumika kwa ajili ya ujenzi wa miradi iliyokusudiwa na si vinginevyo.
Waziri Mkuu alisema ni lazima wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa
Halmashauri wahakikisha viwango vya ubora wa miradi inayojengwa katika maeneo
yao kuwa inalingana na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.
Wakati huo huo Waziri Mkuu amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwenda wilayani Mpanda na kuangalia namna
ya kuipanua hospitali ya Manispaa ya Mpanda ambayo inahudumia mkoa wote wa
Katavi.
Alisema hospitali hiyo ilijengwa mwaka 1957 kama zahanati ambayo
kwa sasa yanatumika katika kuwahudumia wananchi wate wa mkoa huo imezidiwa
hivyo alimuagiza mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga
kuharakisha ujenzi wa hospitali ya mkoa.
Aidha, Waziri Mkuu alisema kuwa wakati mkoa ukiwa kwenye
harakati za ujenzi wa hospitali ya mkoa wilaya nazo zianze ujenzi wa hospitali
za wilaya ili kuhakikisha sera ya Serikali ya kuwa na hospitali katika kila
wilaya inatekelezwa.
Alisema kwa sasa madaktari na wauguzi wanaofanya kazi kwenye
hospitali ya Manispaa ya Mpanda wamezidiwa kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya
wagonjwa kuliko uwezo wao. Hivyo amewataka madaktari na wauguzi wa wilaya ya
Mpanda kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzao wa Manispaa.
Awali hospitali hiyo ilikuwa chini ya uongozi wa halmashauri ya
Mpanda. Hospitali hiyo kwa sasa ipo chini ya Manispaa ya Mpanda hivyo Waziri
Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa huo kuboresha huduma kwa kupeleka dawa na vifaa
tiba vitakavyoweza hospitali hiyo kuhudumia wagonjwa wa mkoa.
Mkoa umetenga sh. bilioni 1.7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa
hospitali ya mkoa.
Habarik zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments