UKOSEFU WA MAJI,VITUO VYA AFYA,BARABARA MBOVU NA WATOTO KUTEMBEA KWENDA SHULENI UMBALI MREFU VYAENDELEA KUWATESA WANANCHI VIJIJI VYA TUMAINI NA ITENKA
Vifusi vya udongo vilivyopo barabara inayotoka Kijiji cha Itenka kuelekea Kijiji cha Tumaini inayokarabatiwa(PICHA NA.Issack Gerald |
Kisima cha maji kilichopo Shule ya msingi Itenka kinachotegemewa pia na wananchi(PICHA NA.Issack Gerald) |
Maji yanayotumika kwa kunywa na shughuli nyinginekijiji cha Tumaini |
Wanawake kijiji cha Tumaini wakichota maji maji wakieleza kuwa ni ya kunywa(PICHA NA.Issack Gerald) |
Bw.Bulu Bukwaya Mwenyekiti kijiji cha Tumaini(PICHA NA.Issack Gerald) |
Bw.Marco Katambi mwenyekiti wa kijiji cha Itenka A(Picha na Issack Gerald) |
Na. Issack Gerald Bathromeo
Wakazi wa vijiji vya Tumaini na
Itenka A vilivyopo kata ya Itenka Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo,wameiomba
serikali kuwatatulia changamoto mbalimbali zinazowakabili zikiwemo ukosefu wa
maji safi na salama,ukosefu vituo vya afya pia mindombinu mibovu ya barabara iliyopo.
Wakazi hao wakizungumza katika vijiji
hivyo,wamesema ni wakati wa serikali kutekeleza ahadi ilizoziahidi wakati wa
kampeni za uchaguzi na kutambua kuwa huduma ya maji na afya ni wajibu wa
serikali kuwapelekea wananchi.
Kwa upandewake mwenyekiti wa kijiji
cha Tumaini Bw Bulu Bukwaya pamoja na mambo mengine ameiomba Halmshauri ya
Wilaya ya Nsimbo kusambaza vifusi vya udongo vilivyolundikwa barabarani bila
kusambazwa visambazwe ili kupunguza adha wanazozipata wananchi wanaposafiri
kutoka Tumaini kwenda Itenka ambapo vifusi hivyo vinaanzia Itenka kupita kijiji
cha Tuamaini.
Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Itenka
Bw.Marco Katambi amesema kuwa mpango uliopo kwa sasa ni kujenga madarasa katika
shule ya msingi Itenka A pamoja na ujenzi wa kituo cha Polisi kijijini hapo
ambapo kwa mjibu wa mwenyekiti wa kijiji hicho askari hawapo kijijini hapo
kufanya ulinzi mara kwa mara.
Hivi Karibuni diwani wa kata ta
Itenka Bw.Joseph Raulence Mpemba alikiri kuwepo kwa chanagamoto mbalimbali kwa
kata nzima ya Itenka yenye vitongoji 26 ambapo alisema changamoto kubwa zilizopo
ni uhaba wa madarasa kwa shule ya Msingi Itenka,watoto kutembea umbali mrefu
kwenda shule,matatizo ya maji,miundombinu mibovvu ya barabara,Ukosefu wa kituo
cha afya na matatizo ya maji.
Hata hivyo Bw.Mpemba alisema kuwa
katika sekta ya afya zimetengwa Shilingi milioni 70 kujenga kituo cha Afya
kijijini Itenka kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Vijiji hivyo umaarufu wake ni kilimo
cha Mpunga na ufugaji wa ng’ombe
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments