RPC NYANDA KATAVI LEO KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAANDAMANO YA OPARESHENI UKUTA SEPTEMBA MOSI.
Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
KAMANDA
wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ASP Damasi Nyanda leo anatarajia kukutana na
waandishi wa habari Mkoani Katavi kuzungumzia mandamano ya Opareshen Ukuta
yanayoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.
Taarifa
ya kamanda Nyanda ambayo imetolewa kwa waandishi wa habari na Afisa habari wa
jeshi hilo Mkoani Katavi,mazungumzo hayo yanatarajia kufanyika kuanzia majira
ya saa 3:00 asubuhi katika Ofisi ya Kamanda iliyopo makao makuu ya Jeshi la
polisi Mkoa wa Katavi yaliyopo Kata ya Ilembo.
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi mara kwa mara limekuwa
likizungumza na waandishi wa habari ili kutoa taarifa kwa jamii kuhusu masuala
mbalimbali yanayoendelea.
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linatarajia kutoa tamko la
katazo la maandamano ya Oparesheni Ukuta ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa
Wilaya ya Tanganyika kutoa tahadhari kwa watakaofanya maandamano Septemba mosi
mwaka huu ambao alisisitiza kuwa watakaoandamana jeshi la Polisi limejiandaa
kuwadhibiti.
Habarika Zaidi na P5ANZANIA.BLOGSPOT
Comments