MKUU WA WILAYA YA TANGANYIKA AZIAGIZA MAMLAKA ZA ARDHI VIJIJI VYA KAMILALA NA KATUMA KUWEKEANA MIPAKA YA KUDUMU KUONDOA MIGOGORO YA ARDHI.
Na.Judica
Sichone-Tanganyika
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika Mh Saleh Mhando
aziagiza mamlaka za ardhi katika kijiji cha Kamilala na Katuma kuhakikisha
wanaweka mipaka ya kudumu haraka iwezekanavyo ili kuondokana na migogogro ya
ardhi.
Ametoa agizo
hilo wakati akizungumza na wananchi katika vijiji hivyo juu ya mgogoro wa ardhi
unaoendelea katika vijii hivyo ikiwa chanzo ni ukosefu wa mipaka.
Ameahidi
kushughulikia kwa haraka mgogoro huo kabla ya msimu wa kilimo haujaanza ili
mwenye haki aweze kuendelea na shughuli za kilimo na kuwasihi wasijichukulie
sheria mkononi pasipo kufuata sheria.
Nao baadhi
ya wananchi katika vijiji hivyo wamefurahia ujio huo wa mkuu huyo wa wilaya ya
Tanganyika na kuwa hiyo ni moja ya njia ya usuluhishi wa mgogoro huo.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments