ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 70 CHACHANGWA UANZISHWAJI BENKI YA WANANCHI KATAVI,WAZIRI MKUU PINDA APIGIA DEBE WANAWAKE KUPEWA KIPAUMBELE KATIKA BENKI HIYO.
Na.Issack Gerald Bathromeo
Zaidi
ya shilingi Milioni 70 zimechangwa na wadau wa maendeleo Mkoani Katavi kwa
ajili ya kuanzisha BENKI YA WANANCHI MKOANI KATAVI.
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania wa awamu ya NNE(wa kwanza kulia mwenye shati nyeupe) akiwa katika mkutano wa uanzishwaji wa benki ya wananchi Katavi(PICHA NA.Issack Gerald |
Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya nne wa
Tanzania Mh.Mizengo Kayanza Peter Pinda ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyeendesha
harambee na kupata kiasi hicho cha fedha,ametoa rai kwa serikali ya Mkoa wa
Katavi kutoa kipaumbele kwa wanawake Mkoani Katavi kupatiwa fursa ya kunufaika katika benki ya
wananchi inayoanzishwa.
Aidha Waziri Mkuu Pinda ametoa rai
hiyo katika mkutano wa wadau wa maendeleo katika Mkoa wa Katavi ambao
wamealikwa kushiriki katika uanzishwaji wa benki hiyo inayolenga kuinua uchumi
wa mwenye kipato cha chini.
Katika hatua nyingine waziri Mkuu
Pinda amezitaka Halmshauri zote 5 za Mkoa wa Katavi kuhakikisha
wanawashirikisha wadau wa maendeleo katika Halmashauri zao ushirikishwaji
unaokwenda sambamba na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa benki hii.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Meja Jenerali Mstaafu Raphael Mugoya ambaye alikuwa mwenyekiti wa
mkutano wa leo, amesema kuwa benki hii ambayo mchakato wake ulianzishwa mwaka
2014 ukakwama,atahakikisha inakamilika katika kipindi cha uongozi wake mkoani
Katavi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo.
Kati ya kiasi hicho cha fedha,fedha
taslimu iliyopatikana ni zaidi ya Shilingi milioni nne ambapo hata hivyo baada
ya kumalizika kikao hiki cha awamu ya kwanza,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja
Jenerali Raphael Muhuga amesema kuwa wanatarajia kuita mkutano mwingine wa
wadau wa maendeleo utakaoshirikisha wafanyabiashara ili kuchangia kiasi kingine
kwa ajili ya kuwezeshwa kwa benki hiyo kukamilika ifikapo Aprili mwakani 2017.
Mkutano huu pia umefanyika kwa kuwezeshwa na
wataalamu mbalimbali wa masuala ya benki wakiwemo Bw.Rukwaro Senkolo ambaye ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya Benki za Wananchi Tanzania na Evans Maseke
ambaye ni Mshauri Mwelekezi na Mtaalamu wa mambo ya Kibenki ambao walikuwa
wakitoa ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu masuala ya kibenki Tanzania.
Nao baadhi ya wajumbe wa Mkutano
pamoja na kusema kuwa benki hii itamwondolea usumbufu mwananchi anaoupata
kutoka kwa taasisisi nyingine za kifedha kutokana na riba kubwa,wameomba riba
iwe ndogo ili kumwinua kiuchumi.
Mkutano huu umewashirikisha wadau wa
maendeleo ambao ni pamoja na Wakuu wa
wilaya wa wilaya za Mpanda,Mlele na Tanganyika,Wakurugenzi wa Halmshauri 5 za
Mkoa wa Katavi,wakuu wa idara kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi pia
wataalamu kutoka Halmshauri zote za Katavi.
Wadau wengine walioshirikishwa ni
mameneja wa Benki zilizopo Mkoani Katavi,mameneja wa vyama vya ushirika mkoani
Katavi,viongozi wa dini,viongozi wa vyama vya siasa,Meneja Chama kikuu cha
Ushirika LATCU,wafanyabiashara,wabunge wote 8 wa Mkoani Katavi, na waandishi wa
habari.
Mkoa wa Katavi unaanzisha Benki ya wananchi kwa kushirikiana na Jumuiya
Ya Benki za Wananchi Tanzania-Community Banks Association of Tanzania (COBAT)
lengo zaidi likiwa ni kupata uelewa pamoja na utaratibu kuhusu manufaa ya kuwa
na benki ya wananchi katika Mkoa wa
Katavi.
Mpaka sasa jumla ya Mikoa 8 kati ya
mikoa 26 ya Tanzania Bara ya Tanzania imekwishaanzisha benki ukiwemo mikoa ya
Kilimanjaro na Kagera.
Zaidi ya wadau wa maendeleo 400
wameshiriki katika mkutano huo.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Endelea kuhabarika na
P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments