MWENGE WA UHURU KUANZA MBIO ZAKE WILAYANI KIBONDO
Leo Mwenge wa uhuru unaanza mbio zake
Wilayani Kibondo mkoani Kigoma.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2016 Bw.George Mbijima(PICHA NA Issack Gerald) |
Mwenge wa uhuru ukiwa Wilayani humo
unataraji kuzindua miradi mbalimbali yenye Thamani ya zaidi ya shilingi
Millioni 900.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya kibondo Bw Saidi Shemahonge amesema mpaka kufikia jana maandarizi ya
kupokea mwenge huo pamoja na miradi itakayo zinduliwa na kuwekewa mawe ya
msingi na mbio za mwenge yalikuwa yamekamilika.
Bw Shemahonge amesema miradi itakayowekewa
mawe ya msingi na kuzinduliwa na mbio
hizo za mwenge ni pamoja miradi iliyo chini ya serikari pamoja na watu
binafisi sambamba na miradi ya vikundi
maalumu hususani vijana na wanawake
Aidha Bw Shemahonge ametoa wito kwa
watu wote ambapo mwenge huo utapita
kujitokeza kwa wingi kuulaki na kusikiliza ujumbe mbalimbali unaotolewa kwa
lengo la kuhimiza maendeleo.
Halmshauri ya Wilaya ya Kibondo ni
miongoni Wilaya 6 zinazounda mkoa wa Kigoma ambapo wilaya nyingine ni BUHIGWE, KAKONKO, KASULU, KIBONDO KIGOMA na UVINZA
Mwandishi: Jastini Cosmas-Kibondo
Mhariri: Issack Gerald Bathromeo
Endelea
kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments