BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO LAFANYA KIKAO CHA MWISHO KUHITIMISHA MWAKA WA FEDHA 2015/2016,MWENYEKITI WA HALMASHAURI ATOA NENO KWA MADIWANI.
Na.Judica
Schone-Nsimbo
Madiwani wa
baraza la Madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo na viongozi wa halmsahauri
hiyo waliopewa dhamana ya kukusanya mapato katika halmashauri hiyo,wametakiwa
kusimamia zoezi la ukuasanyaji wa mapato ili kutumika kwa mujibu wa bajeti.
Rai hiyo
imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya hiyo Mh Raphael Kalinga katika kikao cha mwisho cha
madiwani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 Kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.
Bw Kalinga
amesema mwaka wa fedha 2016/2017 halmashauri imepewa dhima ya ukusanyaji wa
mapato katika maeneo yao,hivyo ni vema kuwa waaminifu katika zoezi hilo kwani
atakayebainika kuhusika na matumizi binafsi ya mapato hayo hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Katika hatua
nyingine Kalinga amewataka baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakiwashawishi
wananchi kutochangia maendeleo katika maeneo yao kuacha mara moja kwani
maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe.
Aidha
ameonya tabia ya baadhi ya watumishi katika halimashauri hiyo wanaotoa huduma
kwa ubaguzi na kupigiwa magoti na wateja wao kuacha mara moja kwani ni haki yao
kupatiwa huduma pasipo usumbufu wowote.
Nao baadhi
ya madiwani katika halmashauri hiyo wamesema
kuwa changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili katika kata na halmashauri zao ni pamoja na akina mama wajawazito
kujifungulia majumbani na chanzo kikiwa ni akina mama kuwategemea zaidi wakunga
waliopo majumbani ambao hawana uwezo mkubwa kwa kitaaluma.
Katika hatua
nyingine,wamesema kuwa wanatarajia kuanzisha chama cha msingi cha ushirika kwa
wakulima wa zao la tumbaku katika Halmshauri ya Wilaya ya ili kuwasiadia
wakulima na kuongeza mapato ya Halmashauri,
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika
Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Comments